Sababu tata ya kimapenzi iliyomfanya Karen Nyamu kusimamishwa kwa muda kwenye tiktok

Alifahamishwa alikuwa amesimamishwa kufanya vipindi vya moja kwa moja kutokana na maudhui yanayochochea ngono.

Muhtasari

•Seneta Karen Nyamu alikuwa akitiririsha moja kwa moja kwenye Tiktok wakati mwanamke mmoja alipomkumbatia.

•Aliambatanisha taarifa yake na screenshot ya ilani ambayo alikuwa amepokea kutoka kwa mtandao huo wa kijamii.

 

KAREN NYAMU
KAREN NYAMU
Image: HISANI

Seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu alisimamishwa kwa muda kutoka kwa vipindi vya moja kwa moja kwenye mtandao wa Tiktok siku ya Jumanne usiku baada ya kupokea kumbatio kutoka kwa mwanamke mmoja.

Mama huyo wa watoto watatu alikuwa akitiririsha moja kwa moja kwenye mtandao huo wa kijamii mwendo wa saa tano usiku kasorobo robo Jumanne usiku wakati mwanamke mmoja alipomkumbatia.

Kisha alipokea taarifa kwamba uwezo wake wa kufanya vipindi vya moja kwa moja kwenye mtandao huo ulikuwa umesimamishwa kwa dakika kadhaa.

"Ninapenda vidhibiti na ukaguzi ambao tiktok imeweka. Mwanamke mmoja alitokea kunikumbatia kwenye kipindi changu cha moja kwa moja na hili likatokea,” Karen Nyamu alisema kupitia akaunti yake ya Instagram.

Aliambatanisha taarifa yake na picha ya skrini ya simu ya ilani ambayo alikuwa amepokea kutoka kwa mtandao huo wa kijamii.

"Tiktok itabanniwa nchini Kenya nikiwa bafu nikioga," aliongeza.

Kulingana na screenshot aliyochapisha, uwezo wake wa kufanya vipindi vya moja kwa moja kwenye mtandao wa tiktok ungerejeshwa saa tano na dakika 29  usiku wa Jumanne baada ya kusimamishwa saa nne na dakika 47 usiku huo.

Mzazi mwenza huyo wa mwimbaji Samidoh pia alipokea taarifa kwamba alikuwa amesimamishwa kufanya vipindi vya moja kwa moja kutokana na maudhui yanayochochea ngono.

"Kwa kuzingatia utofauti wa jumuiya yetu ya kimataifa, haturuhusu maudhui yanayoonyesha au kukuza shughuli au huduma za ngono, au uchi," Tiktok ilimwarifu Bi Nyamu.

Seneta huyo wa kuteuliwa ambaye maisha yake yamejawa na drama nyingi ni miongoni mwa wanasiasa wa Kenya ambao ni maarufu sana kwenye mtandao wa kijamii wa Tiktok.

Bi Nyamu ana zaidi ya wafuasi laki nne kwenye jukwaa hilo na maudhui yake yamekusanya zaidi ya likes milioni nne kufikia sasa.