"Ashamaliza na dakika mbili!" Ghost ashangazwa na kasi ya Gidi katika kula samaki

Mtangazaji mwenza huyo alikejeli kasi ya Gidi katika kula samaki akidai kwamba ilikuwa imemchukua dakika chache sana.

Muhtasari

•Gidi alichapisha video ya mkutano wao wa chakula ambapo wote walionekana wakifurahia mlo wa ugali, samaki na sukumawiki.

•Gidi alijaribu kujitetea akidai kuwa alifika mapema kuliko yeye, hivyo alitarajiwa kumaliza mbele yake.

wakifurahia chakula cha mchana.
Watangazaji Gidi na Ghost wakifurahia chakula cha mchana.
Image: INSTAGRAM// GIDI OGID

Siku ya Jumanne, watangazaji maarufu wa kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi, Gidi Gidi na Jacob Ghost Mulee walikutana katika hoteli moja ili kula chakula cha mchana pamoja.

Gidi alichapisha video ya mkutano wao wa chakula ambapo wote walionekana wakifurahia mlo wa ugali, samaki na sukumawiki.

Video hiyo ilianza huku Ghost akianza kula mlo wake wakati Gidi kwa upande mwingine akiwa tayari amekula sehemu kubwa ya mlo wake, jambo ambalo lilimfanya kocha huyo wa zamani wa Harambee Stars kumfanyia mzaha.

Mtangazaji mwenza huyo mcheshi alikejeli kasi ya Gidi katika kula samaki akidai kwamba ilikuwa imemchukua dakika chache sana.

“Leo niko na Gidi, angalia kasi ya kula Samaki. Angalia, jamaa ashamaliza Samaki na dakika mbili,” Ghost alisema kwa madaha.

Gidi alijaribu kujitetea akidai kuwa alifika mapema kuliko yeye, hivyo alitarajiwa kumaliza mbele yake.

"Anatoka kijijini. Wewe ni Mkamba hii si chakula yenu. Ingekuwa ni muthokoi ungemshinda,” mwanamke aliyekuwa akirekodi video hiyo alisikika akimwambia Ghost huku akimtetea Gidi.

Gidi pia alifanya mzaha kuhusu jinsi mtangazaji mwenzake alivyokuwa akila samaki akisema, “Ni kama hajawahi kula Samaki, ona. Anakula Samaki kama Muthokoi.

Watangazaji hao wawili ambao pia ni marafiki wakubwa wamefanya kazi pamoja kwa zaidi ya mwongo mmoja na nusu.

Mapema mwaka huu, wakati ulimwengu ukiadhimisha siku ya redio duniani, Gidi alisherehekea ushirikiano wake na  ‘Ghost’ Mulee.

Katika taarifa yake, mwanamuziki huyo wa zamani alibainisha kuwa ushirikiano wa utangazaji wa redio ni kama ndoa akidokeza kwamba watangazaji wenza wanapaswa kufahamiana na kukabiliana na kila mmoja, jambo ambalo yeye na Ghost wamefanikiwa kufanya vizuri kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu.

"Ushirikiano wa utangazaji wa redio ni kama ndoa, huwezi kutoboa ikiwa huwezi kukabiliana na ujinga wa kila mmoja!," Gidi Ogidi alisema kupitia mtandao wa Facebook.

Aliambatanisha taarifa yake na picha nzuri zake na Ghost wakiwa studio.

"Imekuwa miaka 16 ya redio ya asubuhi na rafiki yangu Ghost Mulee," aliongeza.

Mtangazaji huyo mahiri wa redio pia alichukua fursa hiyo kuwatambua mamillioni ya mashabiki wao na kuwathamini kwa sapoti yao inayoendelea.

“Asanteni kwa mashabiki wetu wote kwa kusikiliza. Heri ya Siku ya Redio Duniani,” aliandika.