Anahitaji msaada,'Wakenya wasema baada ya Kimani Mbugua kutishia anaowadai mitandaoni

Katika video nyingine, anawakemea Wakenya na katika nyingine anadai kulipwa na wale anaowadai la sivyo atachukua hatua.

Muhtasari
  • Kimani aliingia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akidai pesa kutoka kwa watu anaowadai akitishia kuchukua hatua ikiwa wangeshindwa kulipa pesa hizo.
Aliyekuwa mtangazaji wa Citizen TV Kimani Mbugua
Kimani Mbugua Aliyekuwa mtangazaji wa Citizen TV Kimani Mbugua
Image: Instagram

Aliyekuwa mtangazaji wa televisheni na redio Kimani Mbugua amewaacha baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wakiwa na wasiwasi kuhusu afya yake baada ya  vitisho mtandaoni siku ya Jumatano.

Kimani aliingia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram akidai pesa kutoka kwa watu anaowadai akitishia kuchukua hatua ikiwa wangeshindwa.

Kimani Mbugua anajulikana kuwa amekuwa akipambana na ugonjwa wa Bipolar na hii si mara yake ya kwanza kuzuka kwenye mitandao ya kijamii.

Chapisho lake la Jumatano akiwatishia anaowadai liliwatia mshabiki wake wasiwasi huku wengi wakimshauri afanyiwe maombi na wengine wakisema kwamba Kimani anahitaji msaada.kuhusu afya yake na jinsi anavyotumia mitandao yake ya kijamii.

Alichapisha picha ya orodha ya simu ambazo alifikiri serikali iliwahi kumfuatilia.

Kwenye nukuu, aliandika, "Hizi zote ni simu zilizonunuliwa na GoK ili kufuatilia mawasiliano yangu. Nimezinasa. Ninakuja kwa kila mmoja wenu. Lazima watu wakule pamba.

Katika video nyingine, anawakemea Wakenya na katika nyingine anadai kulipwa na wale anaowadai la sivyo atachukua hatua.

” Iwapo unadaiwa pesa ni bora utume sasa kwa sababu nina bunduki za kulinda pesa zangu, mimi nitakusafirisha binguni wacha vitisho baridi za @williamsamoeiruto” nukuu yake ilisema.

Hii si mara ya kwanza kwa Kimani kuangaziwa kwani mwezi mmoja uliopita alidai kuwa simu yake iliibiwa alipokuwa matembezini asubuhi.