Covid-19: Watu 823 wapona,368 wamepatikana na maambukizi ya corona

Muhtasari
  • Kati ya maambukizi hayo 340 ni wakenya huku 28 wakiwa raia wa kigeni,185 ni wanaume huku 183 wakiwa wanawake
Waziri Mutahi Kagwe
Waziri Mutahi Kagwe
Image: MOH

Watu 368 wamepatikana na maambukizi ya corona nchini kutoka kwa sampuli 6,003 chini ya saa 24 zilizopita.

Kati ya maambukizi hayo 340 ni wakenya huku 28 wakiwa raia wa kigeni,185 ni wanaume huku 183 wakiwa wanawake.

Idadi jumla ya watu waliopatwa na corona nchini imefika 319,379 na kiwango cha maambukizi cha asilimia 6.1%.

Mgonjwa wa chini ana umri wa miezi 9 huku mwenye umri wa juu akiwa na miaka 100.

Idadi ya sampuli zilizopimwa nchini imefika 3,170,792.

Vile vile watu 823 wamepona,Idadi ya waliopona sasa ni 287,963, 707 wamepona wakiwa wanapokea matibabu wakiwa nyumbani huku 116 wakiruhusiwa kuenda nyumbani kutoka hospitali tofauti nchini.

Hamna mtu ambaye ameaga dunia kutokana na maambukizi ya corona  huku idadi hiyo ikisalia kuwa 5,520.

Kuna wagonjwa 865 ambao wamelazwa hospitalini, 7,762 wamejitenga nyumbani.

Vile vile kuna wagonjwa 46 katika kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU).

Idadi ya watu waliopokea chanjo ya corona imefika 11,345,649.