'Siwezi pata mtoto mwingine,'Lilian Muli afunguka jinsi kuwa mama kumebadilisha maisha yake

Muhtasari
  • Lilian Muli afunguka jinsi kuwa mama kumebadilisha maisha yake
Lillian-Muli-new-look-696x418
Lillian-Muli-new-look-696x418

Mwanahabri maarufu Lilian Muli akiwa kwenye mahojiano na Jalango TV, kwa mara ya kwanza amezungumzia jinsi kuwa mama na mzazi kumebadilisha maisha yake.

Mama huyo wa watoto wawili anasema amelazimika kurekebisha maisha yake kwani yeye ni mama kwa wavulana.

Akiongea wakati wa mahojiano kwenye  Muli alishiriki;

"UKuwa mama kumenifanya nitambue kwamba unapaswa kujaza mapengo."

Huwezi kusema kwa sababu baba ameshikana huwezi kuhudhuria mechi za soka.

Mazungumzo yangu lazima yawe karibu na kile wanachopenda,nimekuwa 'tomboy', 'heels' zilichukua kiti cha nyuma kwa sababu niko nje.

Huku akizungumzia kuwa 'single mother' alisema kwamba amekuwa akifanya kila kitu ili wanawe wasisjie pengo lolote.

"Siwezi jiita 'single mother' kwa sababu nina watu katika maisha yangu, iwe ni kaka zangu au baba yangu. Ninasema ninafanya kila niwezalo kuhakikisha hawahisi pengo kamwe," Alizungumza Lilian Muli.

Kuhusu kama ana mpango wa kupata mtoto mwingine, Lilian alijibu;

"Siwezi kuwa na mtoto mwingine. Nimekuwa nikitamani watoto wavulana, kwa sababu nilikua miongoni mwa wavulana."