Mitandao ya kijamii inaweza kujenga na kuvunja mahusiano-Lilian Muli

Muhtasari
  • Lilian Muli awashauri mashabiki kuhusu mitandao ya kijamii na mahusiano ya kimapenzi
Lilian Muli
Lilian Muli

Lillian Muli kupitia akaunti yake ya Instagram amekuwa akizungumza na mashabiki huku akiwashauri jinsi yakuishi maisha yenye furaha na upendo.

Kupitia kwenye ujumbe wake kwa mashabiki LIlian amesema kwamba  aliwahi kuwa na wanaume ambao walikuwa na magari ya gharama kubwa.

Ni nini kilichovutia sana wakati alikiri kwamba walikuwa wanyenyekevu. Aliendelea kuhamasisha wanawake kuwapa fursa ya kujua utu wao.

Kupitia kwenye chapisho nyingine Lilian aliwauliza wanaume na wanawake kama wanaweza kubali wenzi wao kupenda pocha za wanaume au wanawake wengine mitandaoni.

Alizidi kusema kwamba mitandao ya kijamii inaweza kujenga na kubomo mauhusiano ya kimapenzi.

"Mimi nitapenda picha za mtu yeyote ambaye anapenda lakini, lakini sitazidisha hii mitandao ya kijamii inaweza jenga na kubomoa mahusiano ya mapenzi

Mimi sitaki shida kwa nyumba yangu," Alisema LIlian.