Mwanamuziki Nyota Ndogo ameeleza alichopatana nacho baada ya kushauri rafiki yake mwanamueme kuachana na mpenzi wake kutokana na kile alichotaja kuwa ni malalamishi kutoka kwa jamaa huyo.
Nyota ndogo anayejulikana sana kwa kibao, 'Kuna watu na Viatu' ameonyesha kujutia maneno ambayo alimshauri rafiki yake.
Amesema amejifunza somo kubwa baada ya kushauri mwanamume kukatiza mahusiano na mpenzi wake aliyekuwa analalamika kuhusu.
"Jana rafiki yangu alilalamika kuhusu mpenzi wake kwangu,, Na mimi nikamshauri amuache kwani Hafai kwake" alisema Nyota Ndogo.
Alidokeza kilichomshangaza zaidi ni picha alilochapisha mwanamme huyo huku akiambatanisha na ujumbe kuwa hakuna tumbiri inayoweza kuwatenganisha.
Alishindwa tangu lini akakuwa tumbiri.
"Hakuna nyani anayeweza kututenga!!! Jamani nimekuwa tumbiri.