In Summary

• Khadija Kopa ambaye ni mamake Zuchu, amejibu madai kwenye mitandao kuwa Zuchu anauhusiano wa kimapenzi na staa wa bongo  Diamond Platinumz.

• Naomba muulize Diamond na Zuchu sijui,  kwa sababu suala zima halinihusu...waulize watu wawili wanaohusika.

• Aliselma ikiwa wanachumbiana basi hakuna shinda mradi wao wenyewe wanapendana.

Diamond Platnumz,zuchu na Khadija Kopa

Mwanamuziki wa taarab kutoka Tanzania Khadija Kopa ambaye ni mamake mzazi mwimbaji mashuhuri Zuchu, amejibu madai kwenye mitandao  ya kijamii kuwa Zuchu anauhusiano wa kimapenzi na staa wa bongo  Diamond Platinumz.

Hivi majuzi, habari za Diamond Platnumz kuwa na mahausiano na Zuchu zilitamba kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari.

Kutokana na habari hizo, kituo kimoja nchini Tanzania kilimhoji mama wa Zuchu,Khadija Kopa  kubaini ikiwa yanayosemwa ni kweli ama porojo tu.

Katika mahojiano hayo,Khadija alisema hajasikia watu hao wanauhusiano wa kimapenzi na hata wao wenyewe hawalizungumzia suala hilo. Ila aliwaomba wanahabari wahoji na kusakura pia kubaini ukweli kama upo.

Kulingana naye watu ambao wanapaswa kuulizwa kama wanamahusiano ni wale  wanaohusishwa na mapenzi.

"Naomba muulize Diamond na Zuchu sijui  kwa sababu suala zima halinihusu...waulize watu wawili wanaohusika. ikiwa wanachumbiana basi hakuna shinda mradi wao wenyewe wanapendana, "alisema Kopa

Aliongeza kwamba suala la ndoa  ni baina ya watu wawili kukaa pamoja na kukubaliana wanavyotaka kuishi.

"Unaweza kujua ikiwa mwanamume ana kiwango fulani ikiwa unaishi naye?. Hata kama ningemchukulia kila mwanamume usoni basi nisingeolewa na yule niliyenae. Ningeolewa na wa kiwango changu. Unapoishi nao unajifunza zaidi. Zuchu hajaniambia chochote kuhusu uhusiano huo." Mama mzazi alidokeza. 

 

Mhariri Davis Ojiambo

View Comments