In Summary

•Harvey, mtangazaji maarufu wa Marekani  ambaye anatambulika sana kwa kipindi cha Watch Show ameahidi kumchukua Majigambo kama mpwa wake.

•Imekuwa mojawapo ya malengo yangu kuziba pengo kati ya wamamerika wenye asili ya Afrika

steve harvey akiwa na Elsie Majigambo
Image: hisani

Mcheshi wa Kenya Elsa Majigambo ana mjomba baada ya Mtangazaji wa TV kutoka Marekani Steve Harvey kukubali kumsaidia kwa chochote anachotaka maishani

Harvey, mtangazaji maarufu wa Marekani  ambaye anatambulika sana kwa kipindi cha Watch Show ameahidi kumchukua Majimbo kama mpwa wake.

Majimbo mwenye umri wa miaka 20, alieleze changamoto ambazo watoto wakike hukumbana nazo wakati wanataka kuafikia ndoto zao huku akieleza kuwa familia yake haikuwai mchukulia kama mcheshi.

"Watu wengi kutoka Afrika hawafuati ndoto zao kwa sababu kuna njia fulani ambayo imewekwa kwa ajili yao. Ninafurahi kuwa ninafanya kile roho yangu inapenda kwa sababu ninapata fursa  kuwaonyesha wasichana wa ngozi nyeusi kwamba wanaweza pia kufanikiwa" Majigambo  alieleza Harvey.

Harvey alisema kwamba nia yake nikusaidia kupunguza pengo lililoko baina ya Waamerika weusi na wale wengine jambo ambalo limekuwa kwa muda mrefu.

"Elsia, nitakuchukua kama mpwa wangu. Nitakupa nambari yangu ya simu. Ikiwa unahitaji chochote, ikiwa unahitaji ushauri,ikiwa unahitaji mahali pakwenda, piga simu. Sitaki chochote kikufanyiki. Imekuwa mojawapo ya malengo yangu kuziba pengo kati ya wamamerika wenye asili ya Afrika," alisema Harvey.

 

 

View Comments