In Summary

•Nadia Mukami ameeleza kushangazwa na baadhi ya marafiki zake baada ya wao kuona video ya mpenziwe Arrow Bwoy   iliyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii

•Arrow boy alionekana akimvisha kipusa  moja pete,  kinyume na matarajio ya mashabiki wake kwani walifahamu Nadia  kuwa mpenzi wake ambaye  wanatarajia kufunga ndoa

 

Nadia Mukami na Arrow Bwoy
Image: hisani

Mwanamuziki Nadia Mukami ameeleza kutamaushwa na tabia za baadhi ya watu waliokuwa karibu naye hasa baada ya video kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mpenziwe Arrow Bwoy akimvisha pete mwanamke.   

 Arrow boy alionekana akimvisha kipusa  moja pete,  kinyume na matarajio ya mashabiki wake kwani walifahamu Nadia  kuwa mpenzi wake ambaye  wanatarajia kufunga ndoa naye.

Nadia  hakufumbia macho swala hilo alizungumzia  madai hayo, ambapo alikiri alitumia mtandao wa Google kubaini kama kinachosemwa ni kweli ama ni  uvumi tu.

"Mwanamume alitoka kwa mwanamke... Nimeona ile video ya @arrowbwoy nikaanza kuzigoogle Tafadhali nisaidie dondoo zingine kwenye sehemu ya Maoni," alidokeza. 

Ambapo Arrow Boy alimjibu kwa kusema Nadia aliomuonya  dhidi ya kumpa msongo wa mawazo.

"Nilikushow usi ni stress ntavuka chama Next unaona sasa" alisema Arrow boy.

Kutokana na majibizano baina ya wapenzi hawa wawili, Nadia amedokeza waliokuwa marafiki  wake karibu wameanza kumpotelea.

 

View Comments