Mtangazaji raia wa Tanzania maarufu kama Mwijaku amejitokeza na madai mapya kwa Rayvanny an kinachomzua msanii kuaga Wasafi Record
Kupitia kipindi kimoja cha Runinga nchini humo, Mwijaku amezua madai kwamba kuna kiwango cha pesa ambacho msanii huyo anapaswa kulipa lebo ya Wasafi, ili akubaliwe kuondoka kisheria.
Mwijaku alitaja tetesi ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii za Rayvanny kuondoka Wasafi ni kweli na kitu kinachosubiriwa na wanasheria wa lebo hio ni kuona kama msanii huyo ataweza kulipa fedha alizoagizwa.
Sababu ya pili Mwijaku aliyetaja ni kuwa Rayvanny kama angeondoka Wasafi ingemlazimu kuacha kazi alizozifanya ikiwemo na muziki aliyotoa na leo hiyo.
Vilevile, akaunti za mitandao ya kijamii anazomiliki ingemlazimu kuacha kutumia ikiwemo chaneli yake ya Youtube ambayo inawafuasi wengi.
Ikumbukwe msanii mwingine kutoka lebo hio ya Wasafi aliondoka na kuanzisha lebo yake binafsi ya Konde Boy.
Harmonize aliondoka kwa kile alidai kuwa kukosa kuafikia makubaliano na msanii nguli Diamond kuwa chanzo kuu cha kuondoka lebo hiyo sifika nchini Tanzania.