Rayvanny ashindwa kuondoka Wasafi, Kunani?

Muhtasari

•Mwijaku  amezua madai kwamba  kuna kiwango cha pesa ambazo  msanii  huyo anapaswa kulipa lebo ya Wasafi, ili akubaliwe kuondoka kisheria.

•Tetesi ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii  za Ravyaan ni kuondoka Wasafi ni kweli na kitu kinachosubiliwa na wanasheria wa  lebo hio ni kuona kama msanii huyo ataweza kulipa fedha alizoagizwa

Ravyaan
Ravyaan
Image: Hisani

Mtangazaji  raia wa Tanzania maarufu kama Mwijaku amejitokeza na madai mapya  kwa Rayvanny an kinachomzua msanii kuaga Wasafi Record

Kupitia kipindi kimoja cha Runinga nchini humo, Mwijaku  amezua madai kwamba  kuna kiwango cha pesa ambacho  msanii  huyo anapaswa kulipa lebo ya Wasafi, ili akubaliwe kuondoka kisheria.

Mwijaku alitaja tetesi ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii  za Rayvanny kuondoka Wasafi ni kweli na kitu kinachosubiriwa na wanasheria wa  lebo hio ni kuona kama msanii huyo ataweza kulipa fedha alizoagizwa.

Sababu ya pili  Mwijaku aliyetaja ni kuwa Rayvanny kama angeondoka Wasafi ingemlazimu kuacha kazi alizozifanya ikiwemo na muziki aliyotoa na leo hiyo.

Vilevile, akaunti za mitandao ya kijamii anazomiliki ingemlazimu  kuacha kutumia ikiwemo chaneli yake ya Youtube ambayo inawafuasi wengi. 

Ikumbukwe msanii mwingine kutoka lebo hio ya Wasafi aliondoka na kuanzisha lebo yake binafsi ya Konde Boy. 

Harmonize aliondoka kwa kile alidai kuwa kukosa kuafikia makubaliano na msanii nguli Diamond  kuwa chanzo kuu cha kuondoka lebo hiyo sifika nchini Tanzania.