Wimbo wa 'Kwangwaru' umefikisha views milioni 90 YouTube
•Wimbo wa Kwangwaru umefikisha takribani watazamaji milioni 90 kwenye YouTube.
•Wimbo huo ambao Harmonize amemshirikisha aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz umetinga milioni 90 wiki hii
Wimbo wa Kwangwaru umefikisha takribani watazamaji milioni 90 kwenye YouTube.
Wimbo huo ambao Harmonize amemshirikisha aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz umetinga milioni 90 wiki hii na kuwa wimbo wenye watazamaji wengi kwenye kanda ya Afrika Mashariki.
Harmonize walitoa kibao hicho wakati akiwa anafanya kazi na lebo ya Wasafi.
Kutokana na mkataba wake na Wasafi hatoweza kunufaika na kibao hicho kwani mkataba ulikuwa unaeleza kazi zote za muziki alikuwa amefanya na Wasafi zitasalia kuwa za Wasafi.
Diamond anatarajiwa kupata pesa nyingi kutokana na kibao hicho ambacho kimekuwa kwa majukwaa ya muziki kwa miaka mitatu.
Kwangwaru ulipakiwa kwenye YouTube mnamo Aprili mwaka 2018 ambapo uliibuka kuwa wimbo uliopendwa zaidi hasa na vijana wa kizazi kipya.
Harmonize aliondoka kwenye lebo ya Wasafi na kuanzisha lebo yake ambayo amesajili wasanii na kueneza miziki wake.