Wimbo wa 'Kwangwaru' umefikisha views milioni 90 YouTube

Muhtasari

•Wimbo wa Kwangwaru umefikisha takribani watazamaji milioni 90 kwenye YouTube.

•Wimbo huo ambao  Harmonize amemshirikisha aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz umetinga milioni 90 wiki hii

 

Harmonize na Diamond Platnumz
Harmonize na Diamond Platnumz
Image: hisani

Wimbo wa Kwangwaru umefikisha takribani watazamaji milioni 90 kwenye YouTube.

Wimbo huo ambao  Harmonize amemshirikisha aliyekuwa bosi wake, Diamond Platnumz umetinga milioni 90 wiki hii na kuwa wimbo wenye watazamaji wengi kwenye kanda ya Afrika Mashariki.

Harmonize walitoa kibao hicho wakati akiwa anafanya kazi na lebo ya Wasafi.

Kutokana na mkataba wake na Wasafi hatoweza kunufaika na kibao hicho kwani mkataba ulikuwa unaeleza kazi zote za muziki alikuwa amefanya na Wasafi zitasalia kuwa za Wasafi.

Diamond anatarajiwa kupata pesa nyingi kutokana na  kibao hicho  ambacho kimekuwa  kwa majukwaa ya muziki kwa  miaka mitatu.

Kwangwaru ulipakiwa kwenye YouTube mnamo Aprili mwaka 2018 ambapo uliibuka kuwa wimbo uliopendwa zaidi hasa na vijana  wa kizazi kipya.

Harmonize aliondoka kwenye lebo ya Wasafi na kuanzisha lebo yake ambayo amesajili wasanii na kueneza miziki wake.