Nilikuwa na maEX wengi kuliko mke wangu Size-8, asema DJ Mo

Muhtasari

• Katika mahojiano, DJ Mo alisema kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya awali mengi kuliko mke wake.

• Mkewe Size-8 vilevile alimsifia kwa kuwa mpenzi mwenye anamnunulia zawadi nyingi sana.

Pamoja:Size 8 na DJ Mo

DJ Mo na mkewe Size-8 wamefunguka mengi kuhusu Maisha yao ya faragha katika mahojiano ya kipekee na runinga moja nchini.

Wakizungumza katika mahojiano hayo ambayo yalichukua mkondo wa Q&A, walipoulizwa kati yao nani amekuwa katika Mahusiano mengi, DJ Mo alisema kwamba alikuwa na mahusiano ya kimapenzi ya awali mengi kuliko mke wake.

“Nafikiri ni mimi, kwa kawaida wavulana tuko hivo,” alisema DJ Mo.

Wawili hao walifunguka mengi kuhusu Maisha yao huku Size-8 akisema kwamba mumewe hapendi kukubali makosa yake harakana Mo akisema mkewe ndiye mgumu kukubali makosa.

“Mimi nafikiri ni mke wangu ni mgumu kukubali makosa, kabla yake kukubali makosa, itabidi mmevurutana sana, inachukua mud asana,” alisema DJ Mo.

“Mimi nikiulizwa nitasema mume wangu ndiye mgumu, Mo haezi kusema makos ani yake. Huwa anaona makosa ya mtu kwanza, kwa hiyo lazima urudi chini unyamaze, ujieleze ndio akubali,” alisema Size-8.

DJ Mo alisema kwamba siku yao ya kwanza kuenda date ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na ndio maana akamuomba Size-8 wakuwe na huo mtoko.

“Alijitolea akanipeleka date siku yake ya kuzaliwa,” alisema Size-8