Stevie Wonder azungumza kuhusu kuwa raia wa Ghana

Wonder alisema kupata uraia wa Ghana katika siku yake ya kuzaliwa ni "jambo la kushangaza".

Muhtasari

•Siku ya Jumatatu - siku ya kuzaliwa kwa mwanamuziki huyo wa Marekani akitimiza miaka 74 - alipewa uraia wa Ghana na rais wa taifa hilo.

•Mapenzi ya Wonder na nchi yalichochewa na watu aliokutana nao akiwa huko.

Image: BBC

Mwimbaji-mtunzi mashuhuri wa nyimbo Stevie Wonder ni raia wa Ghana.

Siku ya Jumatatu - siku ya kuzaliwa kwa mwanamuziki huyo wa Marekani akitimiza miaka 74 - alipewa uraia wa Ghana na rais wa taifa hilo.

"Hii ndio, pongezi!" Nana Akufo-Addo alimuambiaWonder aliyejawa na furaha , akimkabidhi mshindi huyo wa Grammy cheti kwenye hafla iliyofanyika katika ikulu ya rais ambapo pia alikabidhiwa keki ya siku ya kuzaliwa yenye bendera ya Ghana juu yake.

Wonder aliambia BBC kwamba kupata uraia wa Ghana katika siku yake ya kuzaliwa ni "jambo la kushangaza".

Nyota huyo alizaliwa na kukulia katika jimbo la Michigan nchini Marekani lakini kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano na Ghana - taifa la Afrika Magharibi maelfu ya maili kutoka nyumbani.

Mnamo 1975, akiwa na safu ya albamu zilizovuma katika jina lake, Wonder alionyesha waziwazi hamu ya kuacha muziki na kuhamia Ghana. Aliamini kwamba ukoo wa mababu zake unaweza kupatikana huko, ripoti zinasema.

Wonder aliendeleakuimba na akabaki Marekanilakini baada ya kuongoza tamasha la muziki la Ghana katika miaka ya 1990, alionyesha tena nia kuhamiahuko.

Katika safari ya baadaye nchini Ghana, Wonder aliandika jumla ya albamu yake ya Conversation Peace na katika mahojiano miaka mitatu tu iliyopita nyota huyo alisema anahamia Ghana ili kuepuka dhuluma ya ubaguzi warangi nchini Marekani.

Mapenzi ya Wonder na nchi yalichochewa na watu aliokutana nao akiwa huko.

Aliiambia BBC kwamba moja ya mikutano hii ilikuwa na marehemu Rais wa Ghana Jerry Rawlings, ambaye katika miaka ya 1990 alimkaribisha katika makao ya rais.

"Nakumbuka marehemu Rais Rawlings, ambaye aliniruhusu kuwa rubani mwenza kwenye ndege," Wonder alisema.