Nimepiga magoti, Dj Mo na wakenya naomba msamaha - Ringtone

Muhtasari

• Msanii Ringtone amemuomba Dj Mo msamaha baada ya kisanga kilichotokea katika uzinduzi wa album ya mwanamuziki Size 8.

• Aidha amesema kwamba yeye ni binadamu wa kawaida asiye mkamilifu na kuwaomba wakenya na watumishi wa Mungu kumsamehe.

 

ringtone apoko
ringtone apoko

Msanii Ringtone amemuomba Dj Mo msamaha baada ya kisanga kilichotokea katika uzinduzi wa album ya mwanamuziki Size 8.

Kupitia video iliyopakiwa katika akaunti ya YouTube ya mwanablogu Nicholas Kioko, Ringtone ameonekana akiwa amepiga magoti huku akiwasihi wakenya kwa ujumla kumsamehe kwa makosa aliyoyafanya katika hafla hiyo.

Ringtone amesema kwamba kupitia kitendo chake watu wengi wamekosa imani na wasanii wa miziki ya injili akisema kwamba yeye pamoja na Dj Mo waliaibisha ufalme wa Mungu.

Aidha amesema kwamba yeye ni binadamu wa kawaida asiye mkamilifu na kuwaomba wakenya na watumishi wa Mungu kumsamehe.

Mwanamuziki huyo ameonyesha kutoridhika kwake kwa kile alichokitaja kuwa Size 8 na Dj Mo hawakumtambua kama mtumishi wa Mungu wakati ambapo makasisi waliitwa jukwaani kuibariki album ya Size 8.

Amewaomba wasanii wa injili kutumia roho mtakatifu ili kusuluhisha mambo badala ya kutumia nguvu nyingi kwa vita.

Kwa sasa inasubiriwa kuona iwapo Size 8 na Dj Mo watakubali kumsamehe Ringtone.