Sababu kwa nini Bahati hakuhudhuria uzinduzi wa albamu ya msanii Size 8

Muhtasari
  • Ni kibao ambacho kinazungumzia misukosuko ambayo wanandoa hukumbana nayo katika ndoa

Siku chache baada ya msanii wa injili Size 8 kuzindua albamu yake siku ya JUmapili, amewachilia kibao ambacho kinavuma sana kwenye mitandao ya youtube.

Ni kibao ambacho kinazungumzia misukosuko ambayo wanandoa hukumbana nayo katika ndoa.

Huku mumewe Size 8,mcheza santuri Mo akizungumzia hafla hiyo alisema kwamba walitumia milioni 3.1 pesa ambazo zilikuwa kidogo.

Pia alisema kwamba kuna baadhi ya wageni ambao walikuwa wamealikwa lakini hawakuweza kufika kwenye hafla hiyo.

“Nimefurahi sana tukio lilienda kwa mafanikio kama tulivyotarajia, tuliwaalika wageni wengi na ni wageni watano tu ambao hawakufika, kwangu hilo ni jambo la kusherehekea, pia niseme kwamba kupanga tukio hilo haikuwa rahisi kiasi hicho. , tulianza kuifanya takriban miezi mitatu iliyopita,” alisema.

Miongoni mwa wageni ambao hawakufika kwenye hafla hiyo ni pamoja na; Willy Paul, Bahati na mkewe Marua na Terence Creative.

"Wote walikuwa wamealikwa lakini halikuwa suala la maisha na kifo. Walikuwa wamehifadhiwa mahali pengine,"Alisema haya akiwa kwenye mahojiano na mpasho.