Simjui wala simtambui Stephen Kasolo - Ringtone Apoko

Muhtasari

• Msanii Rintone amesema kwamba hamjui mwanamuziki Stephen Kasolo, na wala hatambui mchango wake kwenye gemu la burudani humu nchini.

• Ringtone ambaye ameendelea kujitawaza kama mwenyekiti wa muziki wa injili hapa Kenya ameonekana katika siku za hivi karibuni akiwakashifu wasanii wengi akisema kwamba hawana upako wa kuimba miziki ya kiinjili.

Image: INSTAGRAM// RINGTONE APOKO

Msanii Rintone amesema kwamba hamjui mwanamuziki Stephen Kasolo, na wala hatambui mchango wake kwenye gemu la burudani humu nchini.

Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa album ya msanii Size 8, Ringtone alisema kwamba Kasolo ni msanii ambaye hajulikani na kwamba hangetaka kumpa umaarufu kwa kumzungumzia.

Hii inajiri wiki chache baada ya Stephen Kasolo katika mahojiano kusema kwamba hawezi kufanya kolabo na Ringtone kwa sababu hangefaidi chochote na kwamba mitindo yao ya uimbaji ilkuwa tofauti.

Ringtone ambaye ameendelea kujitawaza kama mwenyekiti wa muziki wa injili hapa Kenya ameonekana katika siku za hivi karibuni akiwakashifu wasanii wengi akisema kwamba hawana upako wa kuimba miziki ya kiinjili.

Kwa sasa mashabiki watakuwa wanasubiri kuona iwapo Stephen Kasolo atamjibu ama ataamua kupotezea tu madai hayo.