Kwa nini Jose Chameleone anaichukulia Kenya kama mamake licha ya kuwa mzawa wa Uganda

Alibadilika hadi nafasi ya mwanamuziki mwaka wa 1998 alipohaia Kenya na kushirikiana na Ogopa Deejays, lebo ya rekodi ya Kenya, ambayo ilitoa wimbo wake wa kwanza "Bageya" akimshirikisha msanii wa Kenya Redsan.

Muhtasari

• Muziki wa Chameleone ni mchanganyiko mzuri wa watu wa Uganda, rumba ya Afrika ya kati, zouk, na reggae.

• Tangu kuachiwa kwa albamu yake ya kwanza mwaka wa 2000, Chameleone amezindua jumla ya albamu 13.

• Msanii huyo alisema kwamba atasitisha kusherehekea siku zake za kuzaliwa katika kipindi cha miaka 5 ijayo hadi pale atakapofikisha umri wa miaka 50.

JOSE CHAMELEONE
JOSE CHAMELEONE
Image: HISANI

Joseph Mayanja, maarufu kama Jose Chameleone, msanii kutoka Uganda ameelezea sababu za kukiri kuwa Kenya itabakia kuwa mama yake daima katika historia ya maisha yake.

Msanii huyo ambaye mapema wiki hii alifichua kufikisha umri wa miaka 45, amekuwa akisherehekea kwenye tafrija mbalimbali lakini pia kupitia kurasa zake mitandaoni.

Chameleone alisema kuwa japo Uganda ni kama baba yake, daima Kenya itajinafasi katika maisha yake kama mama, kwani humu ndio safari yake ya muziki ilipoanzia mapema miaka ya 2000s.

“Nawapongeza Jose Chameleone na Joseph Mayanja. Mmoja ni bosi wangu na mwingine ni mvulana kutoka Kawempe hadi duniani. NAJITOA kwenu nyote Uganda ni Baba yangu, Kenya Mama yangu, Tanzania, Sudan Kusini, Zambia, Rwanda, DR CONGO!!! AFRICA - Rest is HITSTORY✌🏾 @45 Nina sababu zote za kushukuru kwa baraka zangu. Alhamdulilah,” Chameleone aliandika kwenye moja ya chapisho lake.

Joseph Mayanja alizaliwa Aprili 30, 1979, kwa Gerald na Prossy Mayanja wilayani Kampala, Uganda, akiwa mtoto wa nne kati ya ndugu wanane.

Muziki wa Chameleone ni mchanganyiko mzuri wa watu wa Uganda, rumba ya Afrika ya kati, zouk, na reggae.

Safari yake katika muziki ilianza mwaka wa 1996 kama DJ katika klabu ya usiku jijini Kampala.

Alibadilika hadi nafasi ya mwanamuziki mwaka wa 1998 alipohaia Kenya na kushirikiana na Ogopa Deejays, lebo ya rekodi ya Kenya, ambayo ilitoa wimbo wake wa kwanza "Bageya" akimshirikisha msanii wa Kenya Redsan.

Kwa miaka mingi, Chameleone ametoa nyimbo kadhaa zilizofanikiwa zikiwemo “Mama Mia,” “Mambo Bado,” “Jamila,” “Kipepeo,” “Bageya,” “Shida za Dunia,” “Bayuda,” na “Njo Karibu.”

Wakati muziki wake ukivuma katika bara zima la Afrika, mashabiki wake wakubwa wanatoka Afrika ya kati, hasa katika nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda na Tanzania.

Tangu kuachiwa kwa albamu yake ya kwanza mwaka wa 2000, Chameleone amezindua jumla ya albamu 13.

Msanii huyo alisema kwamba atasitisha kusherehekea siku zake za kuzaliwa katika kipindi cha miaka 5 ijayo hadi pale atakapofikisha umri wa miaka 50.