Siku ya valentines nitakuwa pekeyangu,hakuna wanawake warembo Kenya-Ringtone

Muhtasari
  • Ringtone alisema kuwa tarehe 14 Februari mwaka huu wakati wa siku ya wapendanao, atakuwa peke yake kwa sababu hakuna wanawake warembo nchini Kenya
ringtone apoko
ringtone apoko

Mwanamuziki wa Injili nchini Kenya, Ringtone, amezua hisia tofauti mitandaoni baada ya kufichua mipango yake ya siku ya wapendanao wiki ijayo.

Sababu yake ilionekana kama tusi kwa wanawake wengi nchini Kenya.

Ringtone alisema kuwa tarehe 14 Februari mwaka huu wakati wa siku ya wapendanao, atakuwa peke yake kwa sababu hakuna wanawake warembo nchini Kenya atakesha nao, kuna uhaba wa wanawake warembo nchini Kenya, alidai.

Ringtone amekuwa single kwa muda mrefu lakini mwanzoni mwa mwaka huu alisema lazima aolewe, amenunua gari aina ya Mercedes Benz yenye thamani ya Ksh 7.5Milioni kwa mwanamke ambaye atamwoa.

Ringtone alisema anatafuta mwanamke mwenye anapenda maombi maishani mwake, mwanamke ambaye ataomba kwa saa saba bila kukoma na ambaye atampa watoto wengi maishani mwake.

"Siku ya wapendanao nitauwa ekeyangu kwa ababu ncchini kenya kuna upungufu wa wanawake warembo na wanaomcha Mungu," Ringtone Aliandika.