Size 8 kutoa wimbo wa kwanza baada ya kuidhinishwa kuwa mhubiri.

Muhtasari

•Msanii wa kike Size 8 amedokeza kuwa atakuwa anachilia kibao tarehe 13 mwezi wa Februari.

•Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aaliandika kwamba tarehe 13 mwezi wa pili, Yesu kristo atakuwa anajidhhirisha kwa mashabiki wake kupitia wimbo atakaouachia siku hiyo.

 Msanii wa kike Size 8 amedokeza kuwa atakuwa anachilia kibao tarehe 13 mwezi wa Februari.

Kupitia ujumbe aliochapisha katika ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo aaliandika kwamba tarehe 13 mwezi wa pili, Yesu kristo atakuwa anajidhhirisha kwa mashabiki wake kupitia wimbo atakaouachia siku hiyo.

“13th February, Christ Revealed,”aliandika Size 8.

Hili pia limeonekana wazi kupitia picha ya pamoja aliyopost mzalishaji wa muziki, Jacky B akiwa na Size 8 studioni mwake, wakionekana kuendeleza mchakato wa kuachilia ngoma.

Ikumbukwe kwamba huu utakuwa wimbo wake wa kwanza kabisa baada ya kuidhinishwa rasmi kama mhubiri, jambo ambalo liliibua maoni tofauti miongoni mwa mashabiki wake. Je atakuwa na utafauti gani ukilinganisha muziki wake wa awali? Ni suala la kusubiri ili tuweke mambo paruwanja.

Size 8 alijitosa katika muziki wa injili kipindi ambacho alikuwa amepenya na kutia fora katika muziki wa kidunia huku akisema kwamba alichukua hatua hiyo ili kuwa karibu na Mungu wake.