Video ya Bahati kitandani akiwa amevalia vazi la Diana Marua la kulala yazua hisia mseto (+video)

Bahati hatimaye alifunua mwili wake na kufichua gauni la kulala la mkewe ambalo alikuwa amevalia.

Muhtasari

•Katika video hiyo, wanandoa hao maarufu walionekana wamelala kitandani pamoja huku wakizungumza kuhusu nguo.

•Diana alimshinikiza mumewe avue nguo zake lakini Bahati aliyeonekana kutoridhika aliendelea kulalamika kuwa amechoka.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Video ya ucheshi ya wanandoa Bahati na Diana Marua iliyokusudiwa kuwaburudisha mashabiki wao imevutia hisia tofauti kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo iliyochapishwa kwenye Instagram, wanandoa hao maarufu walionekana wamelala kitandani pamoja huku wakizungumza kuhusu nguo.

Diana ambaye wakati huo alikuwa akicheza na nywele za mume wake alisikika akimuagiza avue nguo zake.

“Babe vua nguo zangu..,” Diana alisika akimwambia Bahati.

Mwanamuziki huyo wa zamani wa nyimbo za injili kisha aliweka uso wa huzuni kuonyesha kutopendezwa na kile mkewe alikuwa akimwambia afanye.

“Aki babe mi sitaki, nimechoka,” Bahati aliyekuwa amefunika mwili wake alisema.

Diana Marua aliendelea kumshinikiza mumewe avue nguo zake lakini Bahati ambaye alionekana kutoridhika aliendelea kulalamika kuwa amechoka.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za mapenzi kisha alifunua mwili wake na kufichua gauni la kulala la mkewe ambalo alikuwa amevalia.

“Babe ni nini? We si unashindanga ukivaa nguo zangu! Mi nikivaa dress yako siku moja ni shida! Na usiwahi vaa t-shirt zangu,” Bahati alilalamika huku akionekana kuenda kwenye bafu kuvua nguo ya Diana ambayo alikuwa ameivaa.

Diana kwa upande wake alibaki kitandani akicheka sana.

Video hiyo imezua hisia mseto kutoka kwa watumiaji wa mtandao huku wengi wakifurahia mabadiliko ya ghafla katika hadithi ya mchezo huo.

Kundi jingine la watumiaji wa Instagram pia limewapongeza wanandoa hao kwa muungano mzuri kati yao na jinsi wanavyoonekana kuchekesha.

Tazama maoni kutoka kwa baadhi ya wanamtandao; -

Miss.shakes: Again, true definition of marry your best friend.

Sherryajuna: Mawazimu wawili walipendana.

Kanzkanguha: Aky akili yangu wewe.. Hii kufikiria yangu daah chafu mno hivi itaniua siku moja.

Nycewanjeri: ebu asivae atapanua.

Just_tonnie: Yhoo, did not see these coming.

Diana_shish_: If you are thinking what I was thinking when Dee said ‘take off my clothes’ piga like.

Sarah_ace_kim: I didn’t expect that, hilarious wah