Kabi wa Jesus ajitosa siasani, aomba ushauri wa kiti cha kuwania

Muhtasari

• Mwanablogu Peter Kabi almaarufu Kabi wa Jesus ametangaza kujimwaya mwenye ulingo wa siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

• Vile vile Kabi amewataka wafuasi na mashabiki wake kumwambia ni kiti kipi ambacho kinamfaa ili aanzishe mchakato wa kukiwania.

Kabi wa jesus
Kabi wa jesus

Mwanablogu Peter Kabi almaarufu Kabi wa Jesus ametangaza kujimwaya mwenye ulingo wa siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Agosti 9 na kuwataka wakenya wampee ushauri wa nafasi ya siasa ambayo wangependa awanie.

Mwanablogu huyo anayejulikana sana kwa video zake za mtandao wa YouTube ambazo wanafanya na mkewe ambaye pia ni mwanablogu Milly wa Jesus amekuwa mkuza maudhui wa hivi punde kujitosa kwenye siasa baada ya wenzake kutoka kwenye tasnia ya ukuzaji maudhui na utangazaji kutangaza azma ya kuwakilisha watu katika maeneo mbalimbali nchini katika uchaguzi ujao.

Wanablogu na wakuza maudhui wengine mashuhuri ambao wametangaza kuvutiwa na viti mbalimbali katika siasa ya Kenya ni Pamoja na Jalang’o, Mc Jessy, Dorea Chege, Mylee Stacey miongoni mwa wengine.

Kabi ameuliza ushauri wa kiti ambacho wafuasi na mashabiki wake wanaona anaweza na watu wengi wamefurika kwenye post hiyo yake kwenye ukurasa wa Instagram na kutoa maoni mbalimbali ya kuchekesha.

Mkewe Milly wa Jesus amemjibu na kumwambia kwamba anaona ni vizuri awanie kuwa mfalme wa moyo wake kwa sababu yeye atamkubalia moyoni mwake mara moja.

“Wania nafasi katika moyo wangu, mara yote lazima nitakupigia kura kuingia moyoni mwangu,” aliandika Milly

Aidha wakuza maudhui mbalimbali wamefurika kwenye post hiyo na kutoa maoni kuhusu tangazo la Kabi kujiingiza katika siasa.

Unahisi Kabi wa Jesus anafaa kuwania nafasi ipi nae neo lipi katika uchaguzi wa Agosti 9?