Kabi Wajesus na Milly Wajesus wajibu madai ya kutomtunza mtoto wao Taji

Muhtasari
  • Kabi Wajesus na Milly Wajesus wajibu madai ya kutomtunza mtoto wao Taji
Image: INSTAGRAM// MILLY WA JESUS

Milly na Kabi Wa Jesus hatimaye wamerejea Kenya kutoka kwa ziara ya wiki mbili nchini Uturuki.

Wakati wa safari yao, Kabi walishtakiwa kwa kutomjali mtoto wao Taji.

Akizungumza katika mahojiano na Mungai Eve, Milly alisema,

"Anayesema hivyo hatujui, wewe si shabiki wa Wajesus. Uturuki sio sehemu ya mtoto, inahusisha kutembea sana. Wazazi wangapi wameacha watoto wao hata kwa miaka?

Wengine hata huenda kufanya kazi nje ya nchi. Kwetu sisi, tunalenga kuhakikisha maisha ya baadaye ya watoto wetu yatakuwa mazuri, tukae kwa nyumba alafu?" Aijibu Milly Wajesu.

Kabi pia alijibu kwa kusema kama mzazi anajua kinachomfaa mwanawe na hivyo watu wanapaswa kuheshimu hilo.

"Wakati ujao watasema 'mliiingia kwa chumba cha kulala mkawacha Taji kwa muda mrefu sana

Sioni sababu ya tuhuma kwamba tunampuuza Taji, chochote tunachofanya ni kwa maslahi ya mtoto wetu

Nataka kumpa mke wangu uwezo ili nisipokuwepo aweze kuendelea. Sidhani kama tuko mahali ambapo wewe kama mzazi unashauriwa jinsi ya kumlea mtoto wako.

Maadamu unafanya vyema na mtoto wako, nadhani wewe ni mzuri." Kabi alisema.

Huku akijibu uhusiano wake na familia ya msanii Bahati, Kabi alisema kwamba ni marafiki, ila watu wanajaribu kuleta chuki, nahali ambapo hapastahili kuwa chuki.