Willy Paul 'anamdate' Amber Ray? Mashabiki watoa hisia zao

Muhtasari

• Willy Paul amekisiwa kuwa katika mahusiano na mwanasosholaiti Amber Ray.

• Vilevile Pozze alimlimbikizia sifa Amber Ray kwa jinsi ambavyo ni mrembo, anapendeza na kwamba ana hela nyingi zinamwezesha kuishi maisha anayoyataka yeye.

Willy paul
Willy paul
Image: hisani

Madai yameibuka kwamba msanii Willy Paul yupo katika mahusiano na mwanasoshiolaiti Amber Ray,hii  ni kutokana  na ukaribu ambao umeshuhudiwa baina yao kwa siku za hivi karibuni.

Kulingana na video waliyoipakia wote wawili katika kurasa zao za Instagram, walionekana wakicheza densi kwa miondoko ya kimapenzi huku mashabiki wakisema kwamba wanapendeza wakiwa pamoja na kwamba wangefurahi kuwaona wakiwa katika mahusiano.

Vilevile Pozze alimlimbikizia sifa Amber Ray kwa jinsi ambavyo ni mrembo, anapendeza na kwamba ana hela nyingi zinamwezesha kuishi maisha anayoyataka yeye.

Aidha wawili hao wamekuwa katika majukwaa mbalimbali wakichapa kazi kwa pamoja huku wakionekana kuwa na ushirikiano mzuri jukwaani.

Ikumbukwe kwamba katika siku za hivi karibuni, Willy Paul aliwaonya mashabiki wake kukoma kumuita jina ‘mkunaji’kwa kila alikitaja kwamba linampotezea Baraka zake katika muziki. Pozze alipewa jina hilo kutokana na hulka yake ya kuwa na wanawake tofauti na kuwa katika skendo mbalimbali na wanawake, huku akisema kwamba sasa ameamu kubadilika na kuzingatia kujenga kipaji chake cha muziki.

Kwa sasa mashabiki watalazimika kusubiri kuona iwapo Pozze ataweka wazi kama wawili hao wapo katika mahusiano ama ni urafiki tu.