MC Gogo afunguka kuhusu kutongozwa na wanawake wakubwa kiumri kwa zawadi za bei

"Unajua watu wameiva hii town, na ni mbaya it's too much Wanataka kukuiba, wanataka kwenda na wewe" alisema

Muhtasari
  • "Hii Nairobi hakuna mbaya, lakini wakati mwingine wanaamua tu wakusumbue," alishiriki.
  • "eh wanakuambia oh baby boy, baby boy, lakini sasa mimi naonaga ni jokes, naonaga argh hawa wako na jokes sana" aliongeza.
Mc Gogo
Image: MOSES MWANGI

Mtumbuizaji mwenye umri wa miaka 23 Mc Gogo yuko kwenye kazi ambapo mashabiki wake wakubwa ni wanawake.

Hii inamwona akijipata katika kila aina ya hali nao pamoja na ofa za kimapenzi na pesa.

Alizungumza na Mungai Eve mnamo Jumanne, Mei 14 ambapo alishiriki kwa haya;

"Unajua watu wameiva hii town, na ni mbaya it's too much Wanataka kukuiba, wanataka kwenda na wewe"

Alieleza changamoto zinazotokana na hili

"Hii Nairobi hakuna mbaya, lakini wakati mwingine wanaamua tu wakusumbue," alishiriki.

Alieleza kuwa ni ngumu

"Mtu anaweze kukutempt akiwa kwa audience, social media ni Hae, Hi, Handsome"

Kwenye DM's wanawake hata wanataka kufanya booking naye.

"Niliwatumia namba ya Meneja wangu sijui alipataje namba yangu. Lakini meneja wangu hatoi namba yangu. Aliniambia anataka kunibook. Unadhani hiyo booking ilikuwa ukweli?"

Alikuwa ni mwanamke ambaye alitaka kupeleka mambo kwenye ngazi nyingine.

"Alitaka kuniweka kwa malengo mengine. Heh alinidanganya lakini ni sawa, nawapenda bado"

Eve alimuuliza ikiwa wanawake wazee huwa wanamtongoza, naye akajibu kwa kusema ndiyo.

"Hehe amekuwachia Range Rover hapo" na akabadilisha maoni yake Eve alipouliza kama aliwahi kupewa Range Rover"Unakataa aje Range Rover?"

Alijibu kwa kukana "Wacha zako wewe, unaoan huu msichana anatry ku do, but it's okay, No, I've not been given, si nakuambiatuu ati......ni mtu tu ako na ** yake and all that, lakini nina pesa zangu pia, saa mniache tuu ni enjoy pesa yangu, saa hamnitaki mntaka ni enjoy pesa sijafanyia kazi?"

Eve aliuliza tena, "Kwa hiyo umepata wanawake wakubwa kujaribu?"

"eh wanakuambia oh baby boy, baby boy, lakini sasa mimi naonaga ni jokes, naonaga argh hawa wako na jokes sana" aliongeza.

"Uso kwa uso, mara ya mwisho nilipokea nadhani ilikuwa Hornbill. Kuna mwenye akakuja akaniambia niaje, ebu maliza twende home. Kuna mwingine hajawahi kuniambia, nioe ama uni***huyo lakini nilimtenda, alishinda anasema hivo. . Nikamtime, nikatoa sauti, .ehe so club nzima inakutazama" aliendelea kusema jinsi alivyobadilika muda huo

McGogo yuko kwenye uhusiano na mwanamke ambaye alimtambulisha kwa sehemu kwa Wakenya.