In Summary
  • Vanessa, ambaye ni mama wa mtoto wa miezi 6 ameamua kushiriki hadithi yake juu ya safari ya huzuni
  • Aliwataka wanaume na hata kila mtu kukomesha unyanyapaa dhidi ya mfadhaiko, na alisema kuwa kwa sasa anajaribu kupona na ana matumaini mambo yatakuwa sawa
Vanessa Mdee
Image: Hisani

Mwimbaji kutoka Tanzania Vanessa Mdee alipatwa na msono wa mawazo  baada ya kumkaribisha mtoto wake wa kwanza.

Vanessa, ambaye ni mama wa mtoto wa miezi 6 ameamua kushiriki hadithi yake juu ya safari ya huzuni.

Akiwahutubia mashabiki wake, alisema msongo wa mawazo baada ya kuzaa ulimletea madhara licha ya uungwaji mkono anaopata kutoka kwa mpenzi wake, Rotimi.

"Watu wengi hawajui mapambano ya msongo wa mawazo baada ya kuzaa na jinsi ilivyo kuwa mama mpya

Hawajui kwamba nimekuwa na mapambano yangu ya msongo wa mawazo. Nadhani ni jambo ambalo linahitaji kuwa.linazungumziwa  zaidi. Hata kama una msaada mkubwa wa mpenzi wa ajabu, nataka kushiriki safari yangu na wewe," Vanessa Mdee mwenye hisia kali alishiriki.

Vanessa alisema kuwa watu wengi hawaelewi huzuni huu na labda wanapomwona mtandaoni akiwa na furaha hudhania kuwa ana furaha maishani mwake.

Aliwataka wanaume na hata kila mtu kukomesha unyanyapaa dhidi ya mfadhaiko, na alisema kuwa kwa sasa anajaribu kupona na ana matumaini mambo yatakuwa sawa.
View Comments