In Summary

•Muigizaji Carol Sonie amekana madai yaliyoibuliwa kwenye mtandao wa kijamii  kwamba alikuwa anatoka kimapenzi na Mcheshi Profesa.

Carol Muthoni katika studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Muigizaji Carol Sonie amekana madai yaliyoibuliwa kwenye mitandao ya kijamii  kwamba alikuwa anatoka kimapenzi na Mcheshi Profesa.

Sonie aliyekuwa mpenzi wa Mulamwah na mama wa Mtoto mmoja ameelezea kuwa picha ambayo mcheshi huyo alipakia kwenye ukurusa wake wa instagram wakiwa pamoja ilikuwa ya kitambo na wao hawajawahi kuwa kwenye uhusiano.

Profesa alipakia picha hiyo kwenye ukurusa wa instagram baada ya habari kuibuka kuwa Sonie ameachana na mpenzi wake.

Akizungumza na Mpasho, Sonie alikana madai hayo na kueleza kuwa walikutana mara moja tu wakati walikuwa wanashoot filamu.

"Tumekutana mara moja tu wakati huo tulikuwa na Mulamwah, wakati tulikuwa tunashoot filamu. Ni mara hiyo pekee niliyokutana na Profesa, tulipiga picha hiyo kutumia simu ya Mulamwah. Tangu hapo hatujazungumza naye kwa simu,”alisema Sonie. 

Aliongeza kuwa alimpigia simu mcheshi huyo na kumueleza kuwa alifanya kosa kubwa kuweka picha hiyo kipindi ambacho walikuwa wanapitia changamoto kwenye mahusiano yake. 

“Alichukua nafasi hiyo ndiyo maana niliishughulikia, mimi na Mulamwah tulikuwa tunateseka, haikuwa vizuri mtu kujinufaisha kwa yale yaliyokuwa yanatupata, si jambo la kucheka, ni mbaya. Tulizungumza, tuko vizuri sasa.”

 

View Comments