In Summary

• Mtandao wa Instagram umemfungia msanii Kanye West kwa muda wa saa 24 baada ya kupakia madai ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchekeshaji na mwandishi Trevoh Noah.

Rappa Kanye West afungiwa Instagram
Image: TMZ TV (Instagram)

Staa wa Hiphop kutokea Marekani Kanye West anaendelea kukumbwa na masaibu si haba baada ya mtandao wa Instagram kumfungia akaunti yake kwa kile mamlaka hiyo ilisema ni kutumia maneno yasiyofaa.

Kanye West alitofautiana na mchekeshaji Trevor Noah, Pete Davidson na aliyekuwa mkewe Kim Kardashian baada ya Noah kuonya kuwa ugomvi wa wanandoa wa zamani hao utaishia kwenye vita usipositishwa.

Hapo ndipo Kanye West aliingia kwenye Instagram na kumwaga cheche kali dhidi ya Noah, maneno ambayo kulingana na Instagram yanaonesha ubaguzi wa rangi ambao ni kinyume cha sheria za jamii ya mtandao huo.

Kanye anasemekana kupakia picha ya Noah kwenye Instagram yake na kuifuatisha na maneno ya ubaguzi wa rangi dhidi yake baada ya kipindi cha Noah na Davidson kuruka kwenye runinga usiku wa jana ambapo Noah alionya juu ya ugomvi wa West na Kardashian.

Katika kuzungumzia mzozo kati ya Kanye West na Kim Kardashian, Trevoh Noah alilinganisha mzozo huo kama ule wa babake wa kambo kumpiga risasi mama yake, tukio ambalo amelielezea vizuri katika kitabu chake cha ‘Born a Crime’

Aliitaka jamii iache kufanya mzaha kuhusu kutalikiana kwa West na Kardashian na kuonya kwamba hali hiyo ya mzozo wao isipodhibitiwa itaishia katika vita kama ambavyo yalimkuta mama yake.

Kanye ameonekana kuwa nac unyongovu na msongo wa mawazo baada ya Kardashian kushinda kesi ya kutaka kutalikiana na yeye, jambo ambalo West hakuwa analitaka kabisa na sasa hali hiyo inamsababishia kuwa na maadui wengi ambao anakosana nao.

Instagram imemfungia kwqa muda was aa 24 huku ikizidisha uchunguzi dhidi ya maneno aliyoyaandika ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Trevoh Noah.

View Comments