In Summary

Mboya - Nimetoshea kumchumbia Huddah Monroe, sababu alisema anapenda vitu kubwa, ama?

Huddah Monroe, Vincent Mboya
Image: INSTAGRAM

Vincent Mboya ni jamaa aliyepata kuangaziwa zaidi na vyombo vya habari za burudani na udaku mwaka jana kutokana na kutangaza kurudisha shilingi elfu 18 ambazo mtanazaji na mchekeshaji Jalang’o alimpa kama msaada.

Hivi majuzi, jamaa huyo mwenye utata alisema kwamba alipata mtu aliyetaka kumfadhili kwa safari ya ndege nje ya nchi lakini kutokana na kukosa visa ya kusafiria, ilibidi amefadhiliwa safari ya ndege kuenda pwani.

Katika mwambao wa pwani, Mboya amekuwa akipiga na kupakia picha za kujivinjari huku akisema kwamba maisha yake yamebadilika baada ya madai ya kuvamiwa wiki kadhaa zilizopita.

Jumanne Mboya alipakia picha fulani kwenye instastories zake akidai kwamba ametoshea kumchumbia au kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ya mwanasosholaiti Huddah Monroe.

Katika picha hiyo ambayo anaonekana na mwanandani pekee, Mboya anasema sasa ashakuwa vizuri na mkubwa kwa Huddah kwani mwanadada huyo kwa kipindi kimoja alidai kwamba anapenda watu wenye wako sawa sehemu zenyewe.

“Nimetoshea kumchumbia Huddah Monroe, sababu alisema anapenda vitu kubwa, ama?… na siringi by the way,” aliandika Mboya kwenye Instagram yake.

View Comments