In Summary

•Amber Ray  alifichua kwamba haijakuwa rahisi kamwe kumlea mwanawe peke yake bila mwenza.

•Alisema anataka mwanawe akue akijua ukweli wote kuhusu maisha. Aliweka wazi kwamba mwanawe huwa anamuelewa sana.

Image: INSTAGRAM// AMBER RAY

Mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu kama Amber Ray ameweka wazi kuwa siku zote yupo makini linapokuja suala la  uzazi.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua lebo yake mpya, Amber Ray alifichua kwa kawaida yeye ni mama mkali na huwa anamdhibiti sana mwanawe.

"Ata kama mimi ni Amber Ray, mimi bado ni mama. Huwa nadhibiti kila kitu kama mama hadi atimize miaka 18. Mimi huwa mkali sana ikifika ni majukumu ya mama," Amber Ray alisema.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 30 alisema kuna uhusiano mzuri sana kati yake na mwanawe.

Amber Ray hata hivyo alifichua kwamba haijakuwa rahisi kamwe kumlea mwanawe peke yake bila mwenza.

"Ni ngumu sana. Si rahisi kuwa single mother. Lakini tunawezana," Alisema.

Amber Ray alisema anataka mwanawe akue akijua ukweli wote kuhusu maisha. Aliweka wazi kwamba mwanawe huwa anamuelewa sana.

View Comments