In Summary
  • Akihojiwa Jumapili ya Mei 15, Jux alisema ni marafiki wanaojumuika sana
Juma Jux

Mwimbaji wa bongo fleva Juma Jux amezungumzia tetesi kuwa anachumbiana na mwanasosholaiti wa Kenya Huddah Monroe.

Akihojiwa Jumapili ya Mei 15, Jux alisema ni marafiki wanaojumuika sana.

Lakini alipingwa kuhusu uhusiano wao wakati video ya wawili hao yenye kudokeza ilipoibuka mtandaoni. Alicheka na kutikisa kichwa kukataa.

Hakuna kitu kama hicho. Haipo. hiyo ya? Ilikuwa zamani huko hii haihusiki na hapa '

Siku chache zilizopita, Huddah Monroe alikuwa Afrika Kusini na Juma Jux. Kulikuwa na ushahidi wa video kuonyesha walikuwa pamoja.

Lakini katika mahojiano haya ya hivi karibuni, Jux alisema hiyo haimaanishi kuwa wanachumbiana au ni wappenzi.

Walipigwa picha pamoja na wakati mmoja, Monroe pia alionekana akiwa amevaa koti lake alilolipenda zaidi.

Jux sasa anasema kuwa lebo yake ni maarufu sana na labda aliinunua ili kukuza brand yake.

"Mimi nipo kwenye mahusiano na najua Huddah yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwahiyo swala la sisi wawili kuwa wapenzi halijitokezi. Lakini nitalijibu swali hili siku nyingine. Lolote linaweza kutokea."

 

 

 

View Comments