In Summary
  • Amberay azungumzia uhusiano wake na ex wake Jimal

Mwanasosholaiti Amber Ray amefunguka kuhusu uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake, Jimal Marlow.

Akizungumza kupitia ukurasa wake wa Instagram, mama huyo wa mtoto mmoja alizungumza kuhusu kuwa na urafiki na Mwenyekiti wa Matatu Sacco, Jimal Marlow.

Wakati wa kipindi cha maswali na majibu, mwanasosholaiti huyo alithibitisha urafiki wake na Phoina Beauty.

Hapa ndipo mashabiki kadhaa walichukua fursa hiyo kumuuliza maswali kuhusu maisha yake ya kibinafsi.

Mmoja wa wafuasi alimuuliza Amber kama yeye ni rafiki na Jimal Marlow. Amber hakusita kumjibu shabiki wake. Kwenye chapisho alijibu:

"Sawa, singesema sisi ni maadui,"Alijibu Amber.

Ikumbukwe kuwa Amber na Jimal walivuma mitandaoni, na hata mwanasosholaiti huyo kuwa mke wa pili wa mwanabiashara huyo.

 

 

 

View Comments