In Summary

•Harmonize ameapa kuachia wimbo unaohusu mihadarati hiyo haramu katika nchini  Tanzania kabla ya mwisho wa mwezi wa Disemba.

• Pia ametangaza kuwa ataanza kutoza Ksh 5M ili kufanya  collabo na wasanii wengine.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameapa kutunga wimbo kuhusu mmea wa Bangi.

Harmonize ambaye kwa muda mrefu amekuwa wazi kuhusu mapenzi yake kwa bangi ameahidi kuachia wimbo unaohusu mihadarati hiyo haramu katika nchini mwake Tanzania kabla ya mwisho wa mwezi wa Disemba.

"Disemba hii, nisipotengeneza wimbo kuhusu bangi .. nipigeni risasi," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na emoji ya kikohozi, ambacho huwa anatumia kama utambulisho wake katika nyimbo zake nyingi. Kikohozi pia huhusishwa na matumizi ya bangi kwani watumizi wengi hujipata wakikohoa baada ya kuvuta.

Konde Boy kwa kawaida huwa hafichi kwamba yeye ni mtumizi wa mihadarati hiyo. Katika video za nyimbo zake nyingi ameonekana akivuta kinachoaminika kuwa bangi. Pia amewahi kurekodi video zingine nyingi akivuta.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide pia ametangaza kuwa ataanza kutoza Ksh 5M ili kufanya  collabo na wasanii wengine.

"Naanza kutoza kwa collabo, TZS 100M. Sharti ngoma iwe kali. Siwezi kusubiri kumtoza mtu fulani TZS 500," alisema.

Mapema mwaka huu, Konde Boy alidokeza kuhusu mpango wake wa kuanzisha Brand ya sigara. Staa huyo alituma ombi kwa mabwenyenye wa Tanzania kujitolea kushirikiana naye kufanikisha ndoto ya kuanzisha kampuni ya kutengeneza sigara.

Katika taarifa yake, Harmonize alisema kuwa anatafuta mshirika ambaye yupo tayari kuwekeza naye huku akidai ni wengi wanaoisubiri bidhaa yake kwa hamu.

"Nataka mtu ambaye atawekeza vizuri. Tufanye hili pamoja. Hakuna haja ya kufanya hili pekee yangu. Nahitaji ushirikiano mkubwa. Kila mtu anajua kiasi gani mtaa unasubiri hii kitu kwa hamu," Harmonize alitangaza.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alifichua kuwa bidhaa yake itatambulika kama sigara ya Tembo. Alisema kuwa kampuni yake itatengeneza sigara kwa kutumia  tubaku inayolimwa nchini Tanzania.

Tembo cigarrette, tobako linalolimwa hapa hapa Tanzania!! Haya sasa matajiri waingie. Wachina sisi wenyewe tunaweza. Bei mtajipangia wenyewe wanangu," Alisema.

Mwanamuziki huyo aliwataka washirika watakaovutiwa na pendekezo kuwasiliana na wasimamizi wake Chopa , Dkt Sebastian Ndege na Mohamed Mmari almaarufu Mjerumani.

View Comments