In Summary

• WhatsApp walikiri kutokea kwa tatizo hilo ila wakasema limechangiwa na mfumo wa Android.

• Waliahidi kuiandikia Google ambaye ni mmilikiwa Andrid kuliangazia suala hilo la kulitatua.

WhatsApp watupiana maneno na Twitter.
Image: Maktaba

Saa chache baada ya mmiliki wa Twitter kutoa kauli ya kudhalilisha akisema mtandao wa WhatsApp unaomilikiwa na Meta si wa kuaminika, WhatsApp wamejibu kwa kujitetea vikali dhidi ya kauli hiyo.

Vita vya maneno vilianza pale ambapo mhandisi mmoja wa Twitter alipopakia picha ya jinsi WhatsApp ilikuwa inafanya kile aliituhumu kuwa ni kutumia kinasa sauti cha siri kipindi chote ambacho alikuwa amelala.

“WhatsApp imekuwa ikitumia maikrofoni chinichini, nikiwa nimelala na tangu nilipoamka saa 6 asubuhi (na hiyo ni sehemu tu ya kalenda ya matukio!) Nini kinaendelea?” Foad Dabiri, mhandisi wa Twitter aliandika.

Musk aliona hilo kuwa fursa nzuri ya kutupa dhihaka kwa mtandao ambao ni washindani wake katika soko huria la kidijitali.

“WhatsApp si mtandao wa kuaminiwa,” Musk aliandika.

 Hata hivyo, WhatsApp waliona vita hii itawaharibia biashara upande wao kwani watu wengi walifika kwa akaunti ya Musk wakitoa maoni yao kuhusu hilo.

WhatsApp kwa haraka walijibu wakijitetea kwamba hawakuwa wanarekodi Dabiri bali ni tatizo lililokuwa kwa mfumo wa Android. Mtandao huo ulitoa hakikisho kwamba umeshatoa taarifa hiyo kwa mzazi wa Android – Google ili kuchukua hatua na kurekebisha kile ambacho Mhandisi wa Twitter alikuwa anateta.

“Kwa saa 24 zilizopita tumewasiliana na mhandisi wa Twitter ambaye alichapisha suala kwa simu yake ya Pixel na WhatsApp. Tunaamini kuwa hii ni hitilafu kwenye Android ambayo inahusisha vibaya maelezo katika Dashibodi yao ya Faragha na tumeiomba Google kuchunguza na kurekebisha,” WhatsApp walijitetea.

 

View Comments