In Summary

•Karen Nyamu na Samidoh walihudhuria Siku ya Michezo katika shule ya mtoto wao, Sam Muchoki Junior  pamoja.

•Mwezi uliopita, seneta Nyamu alidokeza kuhusu mpango wa kupata mtoto mwingine mmoja na Samidoh.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Wazazi wenza Karen Nyamu na Samidoh walihudhuria Siku ya Michezo katika shule ya mtoto wao, Sam Muchoki Junior  pamoja.

Jumanne, seneta huyo wa kuteuliwa alichapisha picha na video za hafla hiyo iliyojumuisha michezo ambayo iliwahusisha wazazi na watoto.

Alifichua kwamba mwanawe aliibuka nambari mbili katika mashindano hayo lakini alikuwa akikataa matokeo.

"Siku ya Michezo katika shule ya mwanangu na nina wasiwasi kidogo kwa sababu alikataa kabisa kuwa nambari mbili na kukataa medali yake ya pili," Karen Nyamu alisema kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliongezea, "Hii tabia ya opposition tunakemea.

Katika picha alizochapisha Nyamu, Sam Junior alionekana akishindana na watoto wengine uwanjani. Video nyingine ilionyesha Samidoh akiungana na watoto na wazazi wengine katika mchezo. Wote walionekana kufurahia siku hiyo.

Sam Jr ni mtoto wa Karen Nyamu na Samidoh wa kwanza pamoja. Wawili hao pia wana binti pamoja, Taraya Wairimu, ambaye alizaliwa mwaka jana.

Mwezi uliopita, seneta Nyamu alidokeza kuhusu mpango wa kupata mtoto mwingine mmoja na Samidoh.

Wakili huyo ambaye tayari ana watoto wawili na mwimbaji huyo wa Mugithi aliweka wazi kwamba bado hajafunga ukurasa wa kuzaa.

Karen alifichua hayo baada ya mtumiaji wa Instagram kudokeza jinsi wanawe wawili wadogo wanavyofanana na baba yao.

"Yaani uliamua watoto wote wafanane na baba yao," shabiki alisema chini ya chapisho la Karen kwenye mtandao wa Instagram.

Bila kusita, seneta huyo alijibu, "Sijagive up. Najaribu one last time."

Seneta Nyamu amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Samidoh kwa muda mrefu na ingawa wao sio wanandoa rasmi, wawili hao wamebarikiwa na watoto wawili pamoja, mvulana mmoja na msichana mmoja.

Kwa muda mrefu, kumekuwa na mzozo unaodaiwa kuwa kati ya seneta huyo na Edday Nderitu kuhusu ni nani mke bora kwa Samidoh.

Mapema mwaka huu, Edday alimwandikia Samidoh ujumbe mrefu kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akimuonya kwamba hayuko tayari kamwe kulea watoto wao katika ndoa ya wake wengi.

View Comments