In Summary

•Wazazi wenza hao wawili walichapisha picha na video za baadhi ya matukio ya siku hiyo maalum.

•Harmonize alionyesha video ya yeye, baby mama wake, bintiye na mwalimu baada ya kulipa karo ya shule na kuandika:

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize na mzazi mwenzake Official Shanteel walimchukua binti yao Zuuh Konde kwenda kuburudika siku ya Jumapili.

Wazazi wenza hao wawili walichapisha picha na video za baadhi ya matukio ya siku hiyo maalum na kuonyesha kujivunia kwao kwa mtoto huyo wao mdogo.

"Jumapili njema na bosi halisi," Harmonize aliandika chini ya picha ya bintiye akiwa ameshika popcorns ambayo alipakia kwenye Instagram.

Pia alishiriki video za mtoto huyo akiwa ameketi kwenye kiti cha nyuma cha gari lake na nyingine akicheza katika eneo la burudani la watoto.

Shanteel pia alichapisha video hizo kwenye ukurasa wake na kuziambatanisha na emoji ya kuonyesha upendo.

Wakati huo huo, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alidokeza kuhusu hatua ya binti yake kujiunga na shule ya chekechea.

Konde Boy alionyesha video ya yeye, baby mama wake, bintiye na mwalimu baada ya kulipa karo ya shule na kuandika:

"Nifanye nijivunie. Niko hapa kwa ajili yako. Baba anakupenda, sawa ni wakati wa shule," aliandika chini ya video hiyo.

Wiki iliyopita,  aliwashirikisha mashabiki wake kwenye kipindi cha maswali na majibu  ambapo mashabiki walimuuliza maswali mbalimbali ya kibinafsi, ya kimaisha na ya kikazi yakiwemo kuhusu uhusiano wake na Harmonize.

Mmoja wa wafuasi wake alimuuliza kwanini alikubali kupata mtoto na staa huyo wa Bongo ilhali hawakuwa kwenye ndoa halisi. 

"Kwani kuzaa na mtu lazima muwe wanandoa," alijibu.

Shanteel alifichua kwamba bado huwa anawasiliana na mzazi mwenza huyo wake kuhusu masuala ya malezi ya binti yao.

Shabiki wake mwingine alitaka kujua kama anaweza kukubali kuolewa na Harmonize mara tu atakapomaliza kujifurahisha na wanawake wengine.

"Mpaka amalize mizunguko yake mie nitakuwa nishaolewa," alisema.

Pia alibainisha kwamba yuko na mtoto mmoja tu, Zuuh Konde ambaye alipata na Harmonize miaka kadhaa iliyopita.

View Comments