In Summary

•Diana alichapisha picha ya kumbukumbu yao na kumkumbusha Bahati jinsi alivyomtunza vizuri katika takriban miaka sita ya  ndoa yao.

•Diana Marua alijibainisha kama mke bora kwa mwimbaji huyo huku akidokeza kuwa aliangukia kitu kizuri alipomuoa.

Image: INSTAGRAM// DIANA MARUA

Mwanavlogu Diana Marua amejivunia juhudi nyingi alizoweka katika kumsaidia mumewe Kelvin  Bahati kufika mahali alipo.

Siku ya Ijumaa, mama huyo wa watoto watatu alichapisha picha ya kumbukumbu yao na kutumia fursa hiyo kumkumbusha Bahati kuhusu jinsi alivyomtunza vizuri katika takriban miaka sita ya  ndoa yao.

"Bahati ona jinsi nilivyokutunza vizuri alafu unataka kuniaibisha hivyo kwenye video ya leo," alisema chini ya picha hizo alizopakia Instagram huku akizungumzia video ambayo anakusudia kuachia baadaye leo Ijumaa.

Pichani, wawili hao ambao walionekana kujawa na furaha pamoja walivalia vitenge vya bluu na maua ya rangi zingine mbalimbali. Walisimama mbele ya gari aina ya Mercedes ambayo huenda walikuwa wanatumia katika siku hizo.

Diana Marua alijibainisha kama mke bora kwa mwimbaji huyo huku akidokeza kuwa aliangukia kitu kizuri alipomuoa.

"Apataye mke mwema, anapata kitu kizuri, ni wazi, halafu ukanikopesha viatu," alisema.

Huku akijibu, Bahati alisema, "Lakini hizi ni nini ambazo unachapisha. Huyu sio mimi."

Mwezi uliopita, wakati wanandoa hao wakishiriki mazungumzo ya wazi,  Diana alichukua sifa zote kwa mafanikio makubwa ya Bahati.

Diana Marua alimweleza mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili kwamba hangekuwa katika nafasi ambayo yuko kwa sasa ikiwa hangekuja katika maisha yake zaidi ya nusu muongo uliopita.

"Naweza kukuambia kitu? Unajua isingekuwa mimi, leo usingekuwa na nyumba hii. Isingekuwa mimi, usingepata watoto hawa. Isingekuwa mimi, usingekuwa na magari manne yameegeshwa hapa,"  alimkumbusha Bahati.

Mama huyo wa watoto watatu alimweleza mwimbaji huyo kwamba usaidizi ambao amempa ni dhibitisho la kweli la mapenzi.

Bahati hata hivyo alimwomba mkewe aache kuchukua sifa ya Mungu akitaja kuwa mafanikio yake yametokana na neema yake.

"Utukufu wa Mungu u ndani yangu, nina Mungu ndani yangu, kazi za Mungu zipo ndani yangu. Kimsingi nina Mungu ndani yangu. Nikisema nisingekuwa mimi, ni kutoka ndani yangu. Kwa hiyo, usingekuwepo popote bila mimi Bahati. Ungekuwa unateseka. Utukufu wa Mungu ndio umeniangazia," Diana alijibu.

Rapa huyo alionekana kuwatupia vijembe wapenzi wa zamani wa mwimbaji huyo huku alidokeza kwamba wanawake ambao Bahati alikuwa akichagua siku za awali hawangemletea mafanikio makubwa aliyo nayo.

View Comments