In Summary

• Mwanasiasa na wakili Karen Nyamu alijawa na furaha baada ya mwanamme Mjaluo kumpokeza maua ya rangi ya njano

• Rangi ya maua hayo ndiyo iliyomkosha mno, kwani ilikuwa ya manjano, rangi ya chama cha UDA ambacho analenga kupata tiketi ili kuwania nafasi ya seneti

Karen Nyamu akihutubia wafanyibiashara wadogo kutoka kaunti ya Nairobi katika makao ya naibu rais William Ruto mapema mwezi Desemba.
Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Mwanasiasa na wakili Karen Nyamu alijawa na furaha baada ya mwanamme Mjaluo kumpokeza maua ya rangi ya njano kama njia moja ya kumsherehekea siku kuu ya wapendanao Februari 14.

Nyamu ambaye analenga kuwania kiti cha seneti Nairobi alijawa na furaha alipopokezwa maua hayo na kuwashabikia wanaume wajaluo kwamba huwa wanaweza sana ifikapo ni suala la mapenzi na mahaba.

Rangi ya maua hayo ndiyo iliyomkosha mno, kwani ilikuwa ya manjano, rangi ya chama cha UDA cha naibu rais William Ruto, chama ambacho Nyamu ni mfuasi sugu na analenga kupata tiketi ya chama hicho ili kuwania nafasi ya seneti

“Luo men yawa! Lakini luo men mnakuanga mmeshinda! This luopean associate of mine had yellow flowers delivered to me today because UDA. Eti nyar rabuon, mano UDA colors hahaha

Ero kamono ahinya. Sasa msianze kuniita semeji,” Nyamu aliwatania Waluo kwenye Facebook yake.

Sherehe za Valentino zilifana sana  Februari 14 ambapo watu mbali mbali waliwasherehekea wapenzi wao huku Nyamu akikosa mtu wa kumsherehekea kwani fununu za chini kwa chini zinahoji walishatengana na mwanamuziki Samidoh, ila kabla ya siku hiyo kuisha, mwanamme huyo mluo alimpiga bonge la surprise kwa maua ya njano, zawadi ambayo Nyamu aliipokea kwa furaha mno.

 

View Comments