In Summary

• Hivi majuzi, Diamond alifichua kwenye moja ya vesi za ngoma 'Nawaza' kwamba uhasama wake na Alikiba ni kutokana na ujana wa kugombania mashabiki.

Wasanii wakongwe kwenye muziki wa bongo fleva, Alikiba, Nay wa Mitego na Diamond Platnumz
Image: Instagram

Msanii wa kuchana mistari kutoka kundi la Weusi, Ney wa Mitego anayejulikana kama Ney Trueboy amekuwa msanii was aba kutoka ukanda wa Afrika mashariki kuwahi kufanya ngoma na wasanii mahasidi wa tangu jadi Diamond Platnumz na Alikiba.

Ney katika collabo yake ya hivi karibuni na Alikiba inamuweka kwenye rekodi hiyo adimu ambayo wengi wanaitaja kama muujiza kufanya muziki na wasanii hao ambao tangu miaka ya 2009 hawaonani uso kwa uso kutokana na kile Diamond alifichua hivi karibuni kwenye wimbo wake wa ‘Nawaza’ kwamba uhasama wao ulitokana na kugombania mashabiki enzi za ujana wao.

Msanii wa kwanza kabisa kufanikiwa kufanya collabo na wasanii hao wawili alikuwa ni Mr Blue ambaye alifanya collabo na Diamond kwa jina ‘Kiss 2 the Lady’ na kisha baadae akafanya kibao cha collabo na Alikiba kilichokwenda kwa jina ‘Mboga7’

Msanii mkongwe Cheed Benz pia aliingia kwenye rekodi baada ya kufanya collabo na Diamond kwa jina ‘Nalia’ na pia kumshirikisha Alikiba kwenye collabo nyingine kwa jina ‘Far Away’ enzi hizo muziki wa Bongo ulikuwa unafanya jitihada kutusua.

Wa tatu ni msanii Godzilla ambaye alimshirikisha Alikiba kwa kibao ‘Milele’ na kisha baadae akamshirikisha Diamond kwa ngoma ‘Mtoto wa Mama’

Kundi la Navy Kenzo ambao pia inasemekana ni wapenzi walitinga kwenye rekodi hizi ambapo walimshirikisha Alikiba kwa collabo ya ‘Lini’ na kisha baadae wakaja kufanya collabo na Diamond kwa jina ‘Katika’ ngoma ambayo ilifanya vizuri mno kwenye majukwaa mwenge ya kupakua miziki.

Nje ya Tanzania, msanii Lolilo kutoka Burundi alimshirikisha Alikiba kwenye kibao ‘Maneno Matamu’ na pia akamshirikisha Diamond Platnumz kwenye collabo ya ‘Najua’

Katika nambari sita tunampata msanii anayetamba kutoka Nigeria, Patoranking ambaye alishirikishwa na Alikiba kwenye collabo ya ‘Bwana Mdogo’ na kisha mwaka 2019 akashirikisha Diamond kwenye kibao moto kwa jina ‘Love u Die’

Nay anaingia hapo nambari saba kwa kuwahi kumshirikisha Diamond kipindi anaanza kwa jina ‘Muziki gani’ na kisha hivi leo akaachia collabo aliyomshirikisha Alikiba kwa kibao cha ‘Nikikuona’

Ikumbukwe katika orodha hii, hakuna msanii kutoka Kenya wala Uganda ambaye mpaka sasa amefanikiwa kufanya collabo na wafalme hao wawili wenye ushindani mkali katika tasnia ya muziki wa Bongo.

View Comments