In Summary

• Watu mbalimbali walijitokeza kutoa maoni yao kuhusu picha hizo baadhi wakimsuta na Nyanzi akisimama vikali kujitetea kwamba hiyo ni sanaa.

Mwanaharakati Stella Nyanzi akiwa katika chumba cha makumbusho cha Ernst Fuchs nchini Austria
Image: Stella Nyanzi//Facebook

Mwanaharakati mkongwe kutoka Uganda, Stella Nyanzi amezua utani na vicheko kweney mtandao wa Facebook baada ya kupakia picha zake akiwa katika makumbusho jijini Viena, Austria.

Katika picha hizo, Nyanzi anaonekana akiwa katika picha mbali mbali za vinyago vya binadamu uchi huku akidai kwamba anamakinika sana kujifunza kuhusu muonekano wa binadamu uchi.

Mwanaharakati huyo ambaye alikimbilia mataifa ya Uropa kutokana na tofauti zake za kisiasa na rais wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni alisema ziara yake katika makumbusho ya Ernst Fuchs alifurahia kutangamana na sanamu mbalimbali zinazoonesha miili ya binadamu wakiwa uchi wa hayawani.

“Huko Vienna, nilitembelea makumbusho ya kuvutia ya fantasia. Nilikwenda kwenye Jumba la Makumbusho la Ernst Fuchs ambalo lilikuwa na sanaa nyingi za kuvutia: picha, picha za kuchora, sanamu, samani, vyombo na keramik. Nina shauku ya sanaa kuhusu umbo la mwanadamu uchi, ilikuwa nzuri sana kuona sanamu zake za uchi zenye ukubwa wa binadamu hai. Sanaa inaongea!” Nyanzi aliandika kwenye Facebook yake.

Watu mbalimbali walipata kutilia maoni yao kuhusu picha hizo alizopiga akiwa anatagusana na sehemu za siri za sanamu hizo, huku wengine wakimsuta kwa picha hizo na yeye akisimama vikali kujitetea kwamba hiyo ni Sanaa tu.

“Je! watoto wako huchukuliaje kuona mama yao akimshika sehemu nyeti za sanamu mchana kweupe? Huogopi radi?” Mmoja kwa jina Dennis Richuni alimuuliza.

“Nani aliwaogesha watoto wangu walipokuwa watoto?” Nyanzi alijibu.

View Comments