In Summary

• Alisema kuwa yeye ni mtumbuizaji na kuwa aliwacha kuwa mchekeshaji kitambo ndio maana anawakemea wanamuziki kila wakati.

• Omondi alisema kuwa Apple Music walipochagua wasanii wa kuangazia alithibisha kuwa hajakuwa akilalamika bure.

Eric Omondi

Aliyekuwa mchekeshaji wa Churchill Eric Omondi amefichua kuwa yeye hafanyi uchekeshaji kama kazi tena.

Alisema kuwa yeye ni mtumbuizaji na kuwa aliwacha kuwa mchekeshaji kitambo ndio maana amekuwa akiwakemea wanamuziki kila wakati.

Omondi alisema kuwa yeye ni rais wa utumbuizaji wa Africa na kuwa hawezi kuwashauri wasanii wa nchi zingine kabla hajawashauri hawa wa Kenya.

"Kitu watu wanasahau ni kuwa mimi si mchekeshaji, mimi ni mtumbuizaji, kuna tofauti. Nilikuwa mchekeshaji kitambo huku ndiko nyumbani, ila sasa mimi si mchekeshaji," Omondi alisema kwenye mahojiano yake na Mungai Eve.

Aliongeza kuwa amekuwa akihisi sekta ya muziki ya Kenya haiko sawa ila anapojaribu kuwashauri wasanii hao wanamfokea.

Omondi alisema kuwa Apple Music walipochagua wasanii wa kuangazia ndipo alipothibitisha kuwa hajakuwa akilalamika bure.

Alisema kuwa alikuwa akimsifia msanii wa Sauti Sol, Bien Aime Sol na kuwa ndiye pekee aliyeweza kuangaziwa na Apple Music.

"Hakikisha nyumba yako iko sawa kwanza kabla ya kuangazia ya wenyewe, nimekuwa nikiwashauri wasanii hao ila hawakunisikia. Matokeo yametoka wakati ambapo Apple Music waliangazia msanii mmoja tu wa Kenya," mtumbuizaji huyo alisema akifurahia kutochaguliwa kwa hao wengine

Omondi alisema kuwa tukio hilo lilimtetea wasanii wengine walipokosa kuangaziwa kwa sababu ya kutotaka kumsikiliza.

Aliwaahidi watu kuwa atafanya jambo lolote ili kuwazuia mapromota wa Kenya kuwaalika wasanii wa nchi zingine na kuwaandalia hafla.

Omondi alisema anawaonya mapromota wa Kenya dhidi ya kuwaalika wasanii wa nchi za nje kabla ya kushughulikia kinachondelea kwenye sekta ya muziki wa Kenya.

"Imefika mahali tunaongea sana, unajua nikisema kitu nitakifanya.Kama wewe ni promota na utaita Burna Boy na umlipie ndege  na bendi yake,unamlipa pesa ya biashara ya watu watatu, unatumia milioni 6 kwa usafiri pekee, kisha uongeze milioni 2 ya hoteli atakayoishi alafu unamlipa milion 5 na hujui Femi One atafika vipi Meru, eeeeh hafla hiyo haitatendeka,nitahakikisha," Omondi aliwaonya mapromota.

Omondi alisema kuwa sekta ya muziki ya Kenya itainuka stesheni za redio zikianza kucheza nyimbo za wasanii wa Kenya.

 

View Comments