In Summary

• Kauli hii kwa kiasi kikubwa inadokeza mtu aliyetendwa vibaya sana katika darasa la mapenzi na hata kufikia mwisho wa kupenda tena.

Simple Boy adokeza kufa moyo katika mapenzi
Image: InstaGRAM

Msanii Stevo Simple Boy baada ya kimya kirefu tangu mwanadada aliyedhaniwa kuwa mpenziwe kumwaga mtama kwenye kuku wengi kuhusu kile kilichokuwa kikifikiriwa kuwa uhusiano wa kimapenzi, sasa amefunguka kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Simple Boy alipakia picha maridadi kabisa akiwa amepiga bonge la muonekano wa fasheni iliyoutii mwili wake, ili kukamilisha dhana ya ‘kuoga na kurudi soko’ baada ya mapenzi kusambaratika.

Katika picha hiyo, mkali huyo wa Freshi Barida aliachia maneno ya kuonyesha kukata tamaa katika mapenzi kwa kunukuu mshororo mmoja kwenye wimbo wa msanii nguli kutoka Tanzania, Lavalava.

“Akinipenda Mungu inatosha!,” Stevo Simple Boy aliandika.

Kauli hii kwa kiasi kikubwa inadokeza mtu aliyetendwa vibaya sana katika darasa la mapenzi na hata kufikia mwisho kabisa wa kuuweka moyo wake rehani kwa ajili ya kupenda.

Bila shaka huenda ni kweli msanii huyo amefikia hatua hiyo baada ya mrembo Gee kudokeza kwamba alikuwa anafanya mitikasi naye kwa ajili ya biashara tu na wala hawakuwahi kuwa pamoja kimapenzi na msanii huyo kutoka mtaa wa mabanda wa Kibera.

Gee alisema kwamba yeye na Simple Boy wamefikia mwisho wa kiki yao ambayo waliisukuma kwa zaidi ya mwezi mmoja mpaka wengi kuamini kwamba wapo pamoja, haswa baada ya kushiriki katika video yenye maudhui ya harusi – tukio ambalo baadae lilikuja kugundulika ilikuwa ni video ya wimbo mpya wa Stevo, Wedding Day.

Stevo Simple Boy huenda hana bahati katika mapenzi kwani alikutana na msichana huyo wa kiki miezi kadhaa tu baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake wa muda mrefu, mrembo Pritty Vishy. Ila hivi majuzi katika mahojiano na kituo kimoja cha redio, Vishy alidokeza kuwa huenda akarudiana na msanii huyo katika kile alisema kwamba nafasi yake katika maisha ya Stevo ipo pale pale na hakuna atakayeliziba pengo lake.

View Comments