In Summary

• Terence alisema kuwa jambo muhimu kabisa maishani mwake ni kuwa anaweza kuitunza familia yake na kuhakikisha kuwa anawapa mahitaji yao.

Terence Creative
Image: Hisani

Mchekeshaji Terence ni mtu maarufu pekee ambaye amefichua kuwa hayuko miongoni mwa watu maarufu waliojaliwa kuwa na thamani kubwa.

Katika mahojiano yake na Mungai Eve, Terence alisema kuwa yeye na mke wake bado wako kwenye harakati ya kujikimu maishani.

Alisema kuwa jambo muhimu kabisa maishani mwake ni kuwa anaweza kuitunza familia yake na kuhakikisha kuwa anawapa mahitaji yao.

"Thamani yangu nimejaliwa na Mungu. Amenijalia uwezo wa kuhudumia familia yangu ndogo, angalau naweza kuikimu familia yangu kwa raha, kulipa ada ya shule na hata kulipia nyumba yangu ya kukodisha,"Terence alisema.

Alisema kuwa bado hajajua thamani yake kwa ujumla ila anafahamu kuwa hana utajiri ambao watu wengine maarufu wamekuwa wakifichua.

Terence aliongeza kuwa alijifunza kuchanga pesa anazopata kutoka kwa kazi mbalimbali anazofanya ili kufanikiwa kufanya mambo ya kujiendeleza.

Alisema kuwa pesa hizo ambazo alikuwa anakusanya zilimsaidia kujiinua kimaisha na hata kuanza kujenga nyumba.

"Nimekuwa nikiweka pesa, nikikusanya ili niweze kununua kitu. Ukiangalia gari langu, nilikuwa nikikusanya pesa zangu kwa zaidi ya mwaka mmmoja , nilikuwa natuma hata elfu 5 motorhub ili nipate gari hilo," alisema.

Mchekeshaji huyo aliwashauri watu kufanya maendeleo katika maisha yao mapema hata pesa zikiwa kidogo.

Aliongea kuhusu tukio la hivi karibuni la KRG ambapo msanii huyo alisema kuwa thamani yake ni ya bilioni 5.

"Mimi sina thamani bado, sijafika hapo,lakini pia nikipata bilioni 5 mtajua. Sina pesa nyingi vile,zile pesa ambazo mke wangu hukusanya na zangu pia ndizo zinazotusaidia kujenga ," alisema.

View Comments