In Summary

• "Pesa ni nzuri. Nilikuwa na wakati mgumu kuchagua gari gani nitaendesha leo. 

Mwanamuziki Willy Paul ametangaza kwamba amekuwa akikumbwa na changamoto kuchagua gari la kuendesha kati magari yake ya kifahari. 

Katika Instagram yake, alisema staa kama yeye kuwa na hela nyingi ni jambo la kujivunia kwani si rahisi kuwa na matataizo ya kifedha maishani.

"Pesa ni nzuri. Nilikuwa na wakati mgumu kuchagua gari gani nitaendesha leo. Tazama kidogo," Pozee alisema.

Katika video aliyopakia, Pozee alikuwa amevaa nguo iliyofanana na rangi ya gari lake (rangi ya manjano) alilojizawadi hivi majuzi .

Alionyesha nguo zake huku akijigamba kuwa na gari hilo la kifahari.

"Nimfananisha nguo zangu, halafu pia namumunya Strepsils ili kutengeneza sauti yangu. Niite kijana mzuri.. maisha ya kuwa mjaluo," mwanamuziki huyo alisema.

Siku chache zilizopita Pozee alinunua gari la kifahari na baadhi ya wanamitandao kudai kuwa alipaka rangi gari lake la kitambo.

Mwanamuziki huyo alikana madai hayo huku akipakia video ya magari magari yake matatu,kuanzia gari lake la kitambo, la sasa na matatu ili kuwajibu wambea. 

Aliwahimiza wanamitandao kuzoea kuwapongeza wenzao wanapokuwa na mafanikio na kutowaonea wivu.

"Walisema kuwa nilipaka gari langu la kitambo rangi ya manjano. Hapana ndio haya hapa yametulia. Maisha mazuri bila vikwazo, maisha bila utata wowote," Willy Paul alisema .

Alimshukuru Mungu kwa mafanikio yake mwaka huu na kwa kumjalia uwezo wa kujizawadi gari lingine.

 

 

View Comments