In Summary

• Ng'ang'a alimtaja mwanamke huyo kama mwadilifu ambaye wamekuwa wakifanya kazi ya kueneza injili kwa ukaribu muda huo wote.

Ng'ang'a ampa zawadi ya gari mwanamke muumini wa kanisa lake.
Image: Screengrab

Mchungaji James Maina Ng’ang’a kutoka kanisa la Neno Evangelism jijini Nairobi kwa mara nyingine tena ameonyesha ukarimu na moyo wa kutoa baada ya kumpa zawadi ya gari mchungaji mmoja ambaye walikutana miaka kadhaa iliyopita.

Ng’ang’a Jumapili baada ya ibada katika kanisa lake, aliamua kumpa mchungaji wake mdogo wa kike gari dogo jipya kama zawadi na kusimulia kwamba mchungaji huyo amekuwa moja kati ya nguzi muhimu katika kanisa lake kwa miaka mingi tu iliyopita.

Alisema kuwa walikutana na mchungaji huyo aliyemtaja kwa jina Jane miaka 10 iliyopita katika hoteli ya Hilton ambapo kulikuwa na mkutano wa runinga ya KBC.

“Jane ndio tulikutana naye miaka 10 iliyopita hapa Hilton katika mkutano wa KBC, akanisalimia na nikamkaribisha kanisani. Jane hajawahi kosa hapa, tukienda kongamano, yeye na wasichana wengine, wao ndio hutangulia na kutengeneza jukwaa,” Ng’ang’a alisema.

Alisema kutokana na moyo wa kujitolea wa mchungaji huyo, alihisi kuguswa kumpa angalau zawadi kama kutambua fadhila zake kanisani, kwani tayari amewazawidi washirika wengi wa kanisa lake na magari katika siku za nyumba.

Ng’ang’a alimtaka Jane kuandamana na wenzake kwenda nje katika kile kilionekana kama ni tukio walilokuwa wamempangia pasi na yeye kujua.

Walipotoka nje, Jane alikabidhiwa ufunguo wa gari hilo na kutakiwa aingie ndani kulingurumisha, lakini alizidiwa na hisia za furaha mpaka kutokwa na machozi na wakati mmoja akaishiwa na nguvu hadi kuketi sakafuni.

View Comments