In Summary

• "Halafu nitakuwa mweupe? Na vipi nikikumbatiana na mtu make up itabaki kwenye nguo?” Kabu aliuliza.

Simon Kabu mara ya kwanza kupakwa make-up.
Image: Instagram

Mmiliki wa kampuni ya utalii ya Bonfire Adventures, Simon Kabu ameshiriki uzoefu wake mara ya kwanza alipofanyiwa urembo wa usoni maarufu ‘make-up’.

Kabu alishiriki klipu kwenye Instagram yake akifanyiwa utaratibu huo usoni na kusema kwamba ilikuwa mara yake ya kwanza.

Mjasiriamali huyo alifichua kwamba alipiga chafya kwa mfululizo, huku pia akipewa masharti ya kutojaribu kulamba midomo yake kisa amepakwa make-up.

“Mara ya kwanza kupakwa makeup. Nimepiga chafya! Ati Sipaswi kulamba midomo Yangu! Jinsi gani sasa? Mdomo unakauka sababu siwezi kulamba midomo yangu,” Kabu alishangaa.

Katika zoezi hilo, Kabu alionekana akizungumza na mwanadada kwa jina Lulu ambaye alikuwa anampa huduma hiyo.

Kwa udadisi, mfanyibiashara huyo alimuuliza Lulu iwapo atakuwa ‘mweupe’.

“Haya maneno kweli nitaweza ya makeup? Halafu nitakuwa mweupe? Na vipi nikikumbatiana na mtu make up itabaki kwenye nguo?” Kabu alitiririkwa na mfululizo wa maswali.

Kwa siku mbili tangu harusi ya Akothee, familia ya Kabu imekuwa ikitrend mitandaoni baada ya picha kuibuliwa Simon akicheka kwa tabasamu na Betty Kyallo ambaye walikuwa na mazungumzo ya faragha na yeye.

Kwa upande mwingine, mkewe Sarah alionekana pembeni mbali kidogo nao akiwa kama anawafuatilia kwa chukizo kubwa usoni mwake.

Lakini wanandoa hao wamekanusha kuwepo kwa tofauti baina yao na Sara alikiri kwamba hakuwa anafirikia kitu kibaya kwani fikira zake hata hazikuwa katika mazungumzo na mumewe na Kyallo.

Walisema kuwa Kyallo ni rafiki wa familia yao kwa muda mrefu na wala hakuna kitu kibaya kinachoweza kutokea kati yao, Sara akimtaka Kyallo kutomezea picha hiyo kwani hata fikira zake zilikuwa mbali sana na hajui kwa nini kamera zilimnasa akiwa kama amepandwa na hasira kumuona anacheka na mumewe.

View Comments