In Summary

• Iwapo msuada huu utapitishwa  na bunge, mapato kutoka kwa  maudhui ya kidijitali yatatozwa ushuru wa wa asilimia 15.

• Mmoja ambaye amepinga vikali pendekezo hilo ni Rais wa ucheshi  Africa Erick Omondi.

Mcheshi Erick Omondi.
Image: INSTAGRAM

Pendekezo la kuwatoza waunda makala ya kidijitali asilimia 15  halijapokelewa vyema na baadhi ya wadau katika sekta hiyo. 

Wadau hao wakiongozwa na mchekeshaji Erick Omondi wamejitokeza kuukataa msuada huo na kuwasihi wabunge kuutupilia mbali.

‘’Serikali ya Kenya na Bunge, msijaribu kuwatoza ushuru  waunda makala ya kidijitali, hamjawafadhili kitu chochote katika shughuli hiyo, wametumia ubunifu wao kutengeneza akaunti za Youtube na Instagram na kufanya kazi yao bila msaada wowote. Kwa hivyo msijaribu kuwatoza ushuru huo,’’ alisema Erick Omondi.

Erick Omondi aliungwa mkono na mchekeshaji na mjasiriamali Ediie Butta pamoja na Mca Tricky.

Mca Tricky alimkashifu Seneta mmoja licha ya kukosa kutaja jina la seneta huyo kwa kusema kuwa waunda makala ya dijitali hawapaswi kupewa msaada wowote na serikali.

‘’Naungama na wewe Erick. Nilimsikia seneta fulani wa analogue akisema kwamba waundaji wa maudhui hawapaswi kusaidiwa na gafament, basi wasikuje kuwatoza senti chache zinazotolewa na waundaji wa maudhui!!’’ aliandika Mca Tricky.

Sekta ya uundaji makala kwa njia dijitali nchini Kenya inakuwa kwa kasi mno kwa miaka michache iliyopita huku waigizaji wakipata mamia ya maelfu kutoka kwa majukwaa kama vile YouTube, Tik Tok  na Instagram.

Pesa hizi zimevutia  serikali na sasa inataka sehemu ya mapato haya kupitia mapendekezo ya marekebisho ya Mswada wa Fedha wa 2023, mojawapo; kuwa kodi ya malipo yanayotolewa kwa waundaji wa kidijitali.

Iwapo msuada huu utapitishwa  na bunge, mapato kutoka kwa  makala ya kidijitali yatatozwa ushuru wa wa asilimia 15.

Hii inamaanisha kuwa kwa kila laki 100 kutoka kwa mapato ya kutengeneza maudhui katika mitandao ya kidijidati utatozwa ushuru wa 15000.

View Comments