In Summary

• Benzema anadaiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu katika klabu ya Al Ittihad, ambao unatarajiwa kumfanya apate takriban pauni milioni 200 kwa msimu.

Benzemac ataja sababu ya kukubali mkataba mnono wa Al Itihad
Image: Instagram

Karim Benzema alitambulishwa rasmi kama mchezaji wa Al-Ittihad na klabu inasherehekea ujio wake kwa mtindo. Bodi ya timu hiyo ilipokea sajili wao mpya kwa kila aina ya heshima, na kutia saini mkataba wake katika eneo ambalo ni la kifahari kama ikulu ya Uarabuni.

Aliposaini, mamia ya mashabiki na simu zao zinazomulika zilifurika kwenye lango la ukumbi huo. Karim pia alifanya mahojiano na vyombo vya habari rasmi vya klabu ambapo alisema kuwa chaguo lake la Saudi Arabia lilichangiwa zaidi na imani yake ya Kiislamu.

“Kwa sababu mimi ni Muislamu na ni nchi ya Kiislamu. Siku zote nilitaka kuishi huko. Tayari nimekuwa Saudi Arabia na ninajisikia vizuri kuhusu hilo. Muhimu zaidi ni nchi ya Kiislamu, inapendwa na ni nzuri. Nilipokuwa na mazungumzo na familia yangu nilikuwa nasaini na Saudi Arabia, wote walikuwa na furaha sana na hapa nipo, kwangu ndipo ninapotaka kuwa.”

“Salaam Alaikum! Nataka kusema asante sana, natumai, inshallah, tutafanya mambo makubwa. Nilichagua Al-Ittihad kwa sababu ni timu kubwa, wametwaa ubingwa na, bila shaka, wana mashabiki wa ajabu, nitafanya kila niwezalo kuiweka timu katika kiwango cha juu zaidi.”

Ndani yake, alielezea Al-Ittihad kuwa klabu kubwa, pamoja na kuwa na furaha kufika katika ligi ambapo mchezaji mwenzake wa zamani na rafiki Cristiano Ronaldo anamsubiri kama mpinzani. Mfaransa huyo hivi karibuni atawasilishwa mbele ya uwanja uliojaa.

Kuhamia kwa Benzema kwa klabu kongwe zaidi ya michezo nchini Saudi kunakuja nyuma ya msimu wa mafanikio zaidi wa Saudi Pro League kuwahi kutokea, ikiwa na rekodi ya wafuasi 2,249,161 kwenye matuta, na mashabiki wakifuatilia mchezo huo kutoka kwa chaneli na majukwaa 48 tofauti katika nchi 170.

View Comments